• Maelezo ya Jumla
  • Stakabadhi za kazi
  • Stakabadhi za taarifa
  • Stakabadhi za marejeleo
  • Vikao vya awali

Lini: Agosti 14-18, 2023  

Wapi: Hoteli ya Ethiopian Skylight, Barabara ya Uwanja wa Ndege, Addis Ababa, Ethiopia

Kaulimbiu: Kuchukua fursa na kuimarisha ushirikiano ili kukabiliana na changamoto za mazingira barani Afrika 

Kikao cha kumi na tisa cha kawaida cha AMCEN kitafanyika kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 18 Agosti mwaka wa 2023 katika Hoteli ya Ethiopian Skylight mjini Addis Ababa, Ethiopia. Kikao hicho kitajumuisha mkutano wa kikundi cha wataalamu kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 16 Agosti, na awamu ya mawaziri, tarehe 17 na 18 Agosti mwaka wa 2023. Kikao hicho kitafanyika chini ya kaulimbiu: "Kuchukua fursa na kuimarisha ushirikiano ili kukabiliana na changamoto za mazingira barani Afrika". Kikao hicho kitatanguliwa na mkutano wa makundi makuu na washikadau (mashirika ya uraia) utakaofanyika katika ukumbi huo tarehe 12 na tarehe 13 Agosti 2023. 

Lengo la kikao cha kumi na tisa cha AMCEN ni kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi mbalimbali na kuimarisha utekelezaji wa mifumo ya mazingira ya kikanda na kimataifa ili kukabiliana na changamoto za mazingira zinazokabili bara la Afrika. Hii inahusisha kujkuanzia na miradi iliyopo, ikijumuisha kuimarisha wajibu wa taasisi zinazounga mkono utekelezaji wa matokeo ya kikanda na kimataifa. Lengo la sera ya hivi majuzi ya AMCEN ni kufanya sehemu kubwa ya kazi yake kuwa uungaji mkono wa utekelezaji. 

Kikao hicho kitatoa jukwaa la kuimarisha ushirikiano kwa jumla barani Afrika katika ajenda ya kimataifa ya mazingira, ikiwa ni pamoja na katika makongamano mbalimbali ya wahusika wa mikataba ya mazingira, United Nations Environment Assembly (UNEA) na michakato mingine ya kimataifa inayohusiana na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuenea kwa jangwa, uharibifu wa mazingira na wa bayoanuai, na uchafuzi na kadhalika, na kuhakikisha kwamba kanda hii, mbali na kuweza kukabiliana na changamoto katika maeneo pia inatumia fursa zinazojitokeza kuleta maendeleo endelevu barani.

Kikao cha kumi na tisa cha kawaida cha AMCEN kitatoa fursa kwa mawaziri kutoa mwongozo wa sera kwa hafla muhimu za mazingira zijazo, ikijumuisha kikao cha 28 cha Kongamano cha Nchi Wanachama wa Mapatano ya Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC COP28) na Mkutano wa Kilele wa Tabianchi wa Afrika; kikao cha sita cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA-6); kushiriki kwa Afrika katika kuunda chombo cha kisheria cha kimataifa kuhusu uchafuzi wa plastiki (mchakato wa INC); maandalizi ya kikao cha 16 cha Kongamano la Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Jangwa (UNCCD COP16); maandalizi ya kikao cha 5 cha Kongamano la Kimataifa kuhusu Ushughulikiaji wa Kemikali (ICCM5), na jinsi Afrika itakachukulia utekelezaji wa Mfumo wa Kimataifa wa Bayoanuai wa Kunming-Montreal.  

Kikao hiki pia kinalenga kuimarisha zaidi kazi za AMCEN katika mchango wake kwa mazingira na ajenda ya maendeleo endelevu ya kanda. Hii ni pamoja na kushughulikia masuala ibuka ya mazingira, kuimarisha juhudi za ushirikiano na wabia na washikadau, kuimarisha msingi wake wa kifedha (Mfuko wa dhamana wa AMCEN, na mapitio ya mapendekezo ya kuimarisha kanuni zake za uendeshaji, kama itakavyoamuliwa katika kikao cha 18 cha kawaida kinachoendelea, pamoja na mambo mengine.

Ajenda ya muda ya kikao cha mawaziri [ Kiingereza | Kifaransa ]

Ajenda ya muda ya kikao cha mawaziri [ Kiingereza | Kifaransa ]

Ajenda ya mda iliyofafanuliwa ya kikao cha mawaziri [ Kiingereza | Kifaransa ]

Kushiriki kwa Afrika katika Uundaji wa Chombo cha Kisheria cha Kimataifa kuhusu Uchafuzi wa Plastiki, ikijumuisha katika Mazingira ya Baharini. Kiingereza | Kifaransa ] 

Maandalizi ya kikao cha sita cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa la Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa Kiingereza | Kifaransa ]

Madini Muhimu na Nafasi Yake Katika Mabadiliko ya Nishati Barani Afrika - Vipengele vya Mazingira vya Madini Muhimu Barani Afrika atika Mabadiliko ya Nishati Isiyochafua Mazingira Kiingereza | Kifaransa ]

Athari kwa Afrika za Mfumo wa Kimataifa wa Bayoanuai wa Kunming-Montreal Kiingereza | Kifaransa ]

Maandalizi ya Afrika ya Kikao cha 5 cha Kongamano la Kimataifa kuhusu Ushughulikiaji wa Kemikali Kiingereza | Kifaransa ]

Ripoti ya Sekretarieti ya Kipindi cha kuanzia Septemba 2022 hadi Julai 2023 [ Kiingereza | Kifaransa ]

Ajenda ya muda iliyofafanuliwa ya mkutano wa wataalamu Kiingereza | Kifaransa ]

Mfuko wa dhamana wa AMCEN [ Kiingereza | Kifaransa ]

Muhtasari wa habari za kikao cha kumi na tisa cha kawaida cha Kongamano la Mawaziri wa Afrika kuhusu Mazingira Kiingereza | Kifaransa ]

Muhtasari wa habari kuhusu ofisi za AMCEN 1985 - 2023 [ Kiingereza ]

Orodha ya hoteli zinazopendekezwa kwa AMCEN19 Kiingereza ]

Uamuzi uliopitishwa wa Mfumo wa Kimataifa wa Bayoanuai wa Kunming-Montreal Kiingereza | Kifaransa ]

Mkakati na Mpango Kazi wa Umoja wa Afrika wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo Thabiti (2022-2032) Kiingereza | Kifaransa ]

Muhtasari wa habari za kikao cha kumi na tisa cha kawaida cha Kongamano la Mawaziri wa Afrika kuhusu Mazingira Kiingereza | Kifaransa ]

Kushiriki kwa Kundi la Afrika katika Uundaji wa Chombo cha Kisheria cha Kimataifa kuhusu Uchafuzi wa Plastiki, Ikijumuisha katika Mazingira ya Baharini. Kiingereza | Kifaransa ]

Ripoti ya kamati ya majadiliano ya serikali mbalimbali ya kubuni chombo cha kisheria cha kimataifa kuhusu uchafuzi wa plastiki, ikijumuisha katika mazingira ya baharini kuhusu kazi ya kikao chake cha kwanza Kiingereza | Kifaransa ]

Ripoti ya Kongamano la Kimataifa kuhusu Ushughulikiaji wa Kemikali kuhusu kazi ya kikao chake cha nne Kiingereza | Kifaransa ]

Ushirikiano kati ya Mkutano wa Mawaziri wa Afrika kuhusu Mazingira na Mawaziri wa Afrika wa Fedha na Mipango ya Kiuchumi - Muhtasari wa sekretarieti Kiingereza | Kifaransa ]

Kukomesha Uchomaji Taka Hadharani Barani Afrika - Muhtasari wa sekretarieti [ Kiingereza | Kifaransa ]

Matokeo ya Kongamanoa Kumi na Tano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Jangwa:  Muhtasari wa sekretarieti [ Kiingereza | Kifaransa ]