UNEP

Kuripoti ulaghai unaoweza kutokea

Tahadhari kuhusu ulaghai unaodai kushirikiana na Shirika la Mazingira la umoja wa Mataifa 

Shirika la Mazingira la umoja wa Mataifa limefahamishwa kuhusu mawasiliano mbalimbali yanayosambazwa kwa njia ya barua pepe, tovuti mitandaoni, mitandao ya kijamii, ujumbe mfupi na kupitia barua za kawaida au faksi, yakihadaa kwamba yametolewa na, au kwa ushirikiano na Shirika la Mazingira wa la umoja wa Mataifa na/au maafisa wake. Ulaghai huu, ambao unaweza kulenga kupata pesa na/au mara nyingi maelezo ya kibinafsi kutoka kwa wapokeaji wa mawasiliano haya, ni ya ulaghai.  Hakuna taarifa za mtu au za kibinafsi zinazopaswa kutolewa kupitia mawasiliano haya ya akaunti hizi za ulaghai wakati wowote ule.

Shirika la Mazingira la umoja wa Mataifa lingependa kutoa onyo kwa umma kwa ujumla kuhusu shughuli hizi za ulaghai zinazofanywa kwa kutumia jina la Shirika, na/au maafisa wake, kupitia mifumo mbalimbali za ulaghai.

Shirika la Mazingira la umoja wa Mataifa halitozi ada yoyote katika hatua yoyote ya mchakato wake wa kuajiri (kutuma maombi ya kazi, mahojiano, maandalizi, kutoa mafunzo) au ada nyinginezo, au kuomba habari kuhusu akaunti za benki za waotaka kuajiriwa. Ili kutuma ombi la kazi, nenda kwa careers.un.org kisha ubonyeze “Vacancies.” Soma zaidi kuhusu ulaghai unaohusiana na ajira.

Shirika la Mazingira la umoja wa Mataifa halitozi ada yoyote katika hatua yoyote ya mchakato wake wa kutafuta mawakala (usajili wa msambazaji wa bidhaa, uwasilishaji wa zabuni) au ada nyinginezo. Tembelea Kitengo cha Mawakala ili kuona fursa zilizopo katika Umoja wa Mataifa.

Umoja wa Mataifa hauitishi taarifa yoyote inayohusiana na akaunti za benki au taarifa nyingine za kibinafsi.

Shirika la Mazingira la umoja wa Mataifa halitoi nafasi za kazi, matuzo, fedha, vyeti, kadi za benki za kiotomatiki (ATM), ili kufidia ulaghai kwenye Intaneti, ufadhili wa masomo, au maelezo kuhusu mtu ili kujipatia pesa, au kushiriki kwenye bahati nasibu.

Shirika la Mazingira la umoja wa Mataifa haliidhinishi huduma za matibabu, likizo kwa wanajeshi au waliostahafu, au kutoa vifurushi ukitoa pesa.

Shirika la Mazingira la umoja wa Mataifa linapendekeza kwa dhati kwamba wanaopokea maombi, kama yaliyoelezewa hapo juu, wawe waangalifu zaidi kuhusiana na maombi hayo. Kupoteza fedha na utambulisho wako kuibiwa kunaweza kutokana na kuhamisha pesa au kutoa habari za kibinafsi kwa wale wanaotoa mawasiliano kama hayo ya ulaghai. Waathiriwa wa ulaghai kama huo wanaweza pia kuuripoti kwa vyombo vya kisheria vya eneo wanalotoka ili kuchukuliwa hatua mwafaka.

Sio hati rasmi. Inatoa taarifa tu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea ukurasa wetu wa Sera ya Utovu wa Nidhamu na Kupambana na Ulaghai hapa au Ofisi Inayosimamia Huduma za Ndani (OIOS) hapa.