Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa ni la kimataifa na linajumuisha sekta nyingi. Hii inadhihirika kupitia kwa mfumo wake wa utendaji kazi, shughuli zake na kupitia kwa wafanyakazi wake.

Likiwa na makao makuu Nairobi, Kenya, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa linaongozwa na Kikosi cha Viongozi Andamizi ambacho mwenyekiti wake ni Mkurugenzi Mtendaji. Tunafanya kazi kupitia kwa idara, afisi za kimaeneo, zile tunazoshirikiana nazo kutoka nje, pamoja na mtandao unaokua unaojumuisha vituo bora vya ushirikiano. Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa pia ni mwenyeji wa makubaliano, sekritarieti na mashirika baina ya mawakala wa uratibu.