Maswali yanayoulizwa mara kwa mara (FAQS)

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara (FAQS)

KUSHIRIKI NA KUTUMA MAOMBI

"wazo kuu" inamaanisha nini?

Kauli maarufu ya Albert Einstein inasema kuwa: “Hatuwezi kutatua matatizo kwa kutumia mtindo uleule wa kufikiri tuliotumia tulipoyajenga.”  Ndio sababu masuluhisho kwa changamoto kuu zaidi za mazingira huenda yakatoka kwa vijana. Fikra yako mpya na uwezo wa kuwa mbunifu hukupa fursa zaidi kuliko vizazi vilivyotangulia. 

Kwa hivyo wazo lako kuu ni lipi? Inaweza kuwa kampeni nyanjani ya kukuza usafiri wa kiwango cha chini cha hewa ya ukaa; apu nzuri ya kuongeza maarifa kuhusu ekolojia; kampeni ya upandaji miti ili kuboresha maeneo yalioharibiwa; tamasha la sanaa linaloonyesha uzuri wa mazingira; teknolojia ya kuokoa na kuchakata rasilimali adimu za maji; chombo cha kifedha cha kuwezesha upatikanaji wa nishati isiyochafua mazingira; au mtindo mpya ya usimamizi wa malighafi katika jamii.

Wazo lolote ulilonalo, litasionekana wazi iwapo litashughulikia moja kwa moja changamoto za mazingira kama vile uharibifu wa bayoanuai, mabadiliko ya tabianchi, uchafuzi au uhaba wa maji; liwe wazo lako na bunifu; na linaweza kuimarishwa kwa kuzingatia utafiti wa awali. Jitolee kwa dhati na ufikiri kwa njia isiyokuwa ya kawaida. Kuwa kichochezi za mabadiliko chanya!

Je, ni lazima niwe numesomea sayansi ya mazingira au nifanye kazi katika sekta ya mazingira ili kuwa na uwezo wa kushinda?

Hapana. Tunaamini kwamba mtu yeyote ana uwezo wa kuwa Kijana Bingwa Duniani.

Je, ninashindana katika eno lipi duniani?

UNEP inafanya kazi katika maeneo sita:  Afrika, Asia na Pasifiki, Ulaya, Amerika ya Kusini na Karibiani, Amerika Kaskazini, na Asia Magharibi. Nchi yako ya makazi huamua eneo ulimwengu ambalo unashindania tuzo.  Ili kutambua eneo lako, tembelea: http://www.uneplive.org/regionscountries    

Nitakuwa chini ya miaka 18 wakati wa kutuma maombi.  Kwa nini siwezi kutuma maombi ya kushiriki tuzo?

Wakati wako utafika!  Tunajua kwamba umri haujalishi zaidi, na haupaswi kumzuia mtu yeyote kuwa na wazo kubwa au kuleta mabadiliko. Hata hivyo, ili tutambue uwezo wako kama mfanya mabadiliko ya mazingira, tunahitaji kuona ushahidi mkuu katika mfumo wa uzoefu wa maisha na mafanikio ya zamani. Zaidi ya hayo, Vijana Bingwa Duniani watahitajika kusafiri bila kusindikizwa kwa sherehe mbalimbali, warsha za mafunzo na hafla za vyombo vya habari.   

Je, kuna ada ya kutuma maombi? 

Hapana. Hakuna malipo ya kushiriki.

Je, kikundi kinaweza kutuma maombi ya pamoja? 

Tunatafuta kuwatuza watu werevu.  Mawazo yako yanaweza kutoka kwa kazi ya kikundi, au wazo lako kubwa linaweza kuhitaji kikundi kutekelezwa, lakini kutuzwa hatimaye, ushauri na ukuzaji wa shughuli zako utatolewa kwa mtu binafsi na wala sio kwa vikundi. 

Je, ninaweza kutuma maombi zaidi ya mara moja?

Haiwezekani kwa mwaka uleule. Tunakuhimiza uwasilishe tu wazo lako bora zaidi.

JINSI YA KUTUMA MAOMBI YA KUSHIRIKI

Ninawezaje kutuma maombi yangu ya kushiriki?

Unaweza kutuma maombi yako ya kushiriki kupitia tovuti ya kupokea maombi kwenye tovuti hii. Utahitaji kutambua mtu ambaye anaweza kuthibitisha wazo lako linawezekana na kuzungumza juu yako kama mtu binafsi.  Ukishatuma maombi yako ya kushiriki, huwezi kuhariri wala kubadilisha.   

UAMUZI

Je, kuna washindani wangapi?  

Tunatarajia kupokea maelfu ya maombi ya kushiriki katika awamu ya kwanza. Kutoka kwao ambapo watakaohitimu katika kanda wataorodheshwa kutoka Afrika, Ulaya, Amerika ya Kusini na Karibiani, Amerika Kaskazini na Asia Magharibi. Washiriki waliofika fainali kutoka kwa kanda wataamuliwa na Baraza la Kimataifa la Majaji ambapo Vijana Bingwa Duniani saba, wanaowakilisha kila eneo duniani, watachaguliwa.

Nani atakayepitia na kuwekea alama maombi yangu ya kushiriki? 

Wataalamu kutoka UNEP watatathmini maombi yako ya kushiriki. Iwapo utachaguliwa kuwa mmoja wa watu 21 watakaohitimu kutoka kwa kanda, basi utaalikwa kutoa habari zaidi, ikijumuisha video fupi inayozungumzia wazo lako.  Wasifu wako na wazo lako litatumwa kwa Baraza la Majaji linalojumuisha watu mashuhuri walio na tajriba ya masuala ya mazingira.  Baraza hili la majaji litachagua jumla ya Vijana Bingwa Duniani saba wanaowakilisha kila eneo. 

Je, baadhi ya sababu zinazoweza kupelekea maombi uliotuma kukataliwa ni zipi? 

Huenda hujatimiza masharti ya kukuwezesha kushiriki au mtu aliyezungumza kukuhusu hakukidhi vigezo vinavyohitajika. Huenda ulishindwa kuwasilisha kabla ya tarehe ya mwisho.  Au labda haukufikisha alama zinazohitajika.  Vyoyote vile, usikate tamaa.  Tunatoa matuzo saba tu katika shindano la kimataifa linaloshindaniwa vikali.  Kwa sababu hiyo, kutakuwa na miradi mingi bora ambayo haitachaguliwa.   

KUTANGAZWA KWA MATOKEO

Je, matokeo yatatangazwa lini na vipi?

Ikiwa utachaguliwa kama mshindi wa kikanda, utawapokea ujumbe kupitia barua pepe. Vijana Vijana Bingwa Duniani saba watajulishwa kupitia barua pepe a kutangazwa hadharani mda mfupi baadaye.

MATUZO NA USHAURI

Nikishinda, wajibu wangu wa usafiri utakuwa upi?

Ukichaguliwa kuwa Kijana Bingwa Duniani, utahitajika kusafiri katika ngazi ya kimataifa ili kuhudhuria sherehe ya kuwatuza Mabingwa wa Dunia, kambi ya mafunzo kwa wajasiriamali na ziara za kielimu. Tarehe halisi na maeneo yatatangazwa wakati wa programu. Gharama zote za usafiri zitagharamiwa na UNEP.  Washindi wote lazima wawe na pasipoti halali.

Nikishinda, kuna vidhibiti vyovote kwa jinsi ninavyoweza kutumia pesa za tuzo?

Vijana Bingwa Duniani wanatakiwa kutumia mtaji kutokana na ufadhili kutekeleza mawazo yao makubwa. Hatutakuuliza uache kazi yako ya mchana au uache chuo kikuu, lakini matumaini yetu ni kwamba utatumia vizuri mtaji, ushauri wa wataalamu, umaarufu wa kimataifa na ufikiaji wa mitandao mikuu ili kuwa mleta mabadiliko ya mazingira. Pia tutakuomba uwasilishe blogu na video mara kwa mara, na uhamasishe kuhusu mradi wako hadharani ili watazamaji wetu waweze kufuata safari yako kwenye tovuti hii. Washindi pia watahitajika kuwasilisha ripoti ya mwisho na bajeti inayoelezea matumizi ya fedha na mafanikio yao.

Explore More