Tunachotafuta

Tunachotafuta

Ni nini kitakufanya kuwa Kijana Bingwa Duniani?

Mazingira yetu yako chini ya shinikizo na ushahidi uko kila mahali. Uko katika hewa tunayovuta, chakula tunachokula, na maji tunayokunywa. Uko kwenye udongo, mito, bahari na anga zetu.  Wengine huurejelea kama changamoto kuu za nyakati zetu.

Swali ni: Unafanya nini kuhusu hali hii? Sasa kuliko wakati mwingine wowote, sisi tunaojali dunia asilia lazima tusimame kidete na tuigwe. Ikiwa wewe ni mwanaharakati, mwalimu, mvumbuzi au msanii, tunakuhitaji kubadilisha hali iliopo sasa na kupigania afya ya sayari yetu na watu wake.

Ikiwa una wazo kuu la kutunza au kuboresha mazingira; ikiwa una rekodi ya kipekee ya kuchochea mabadiliko; ikiwa hauogopi kushindwa; na ikiwa unaamini kuna mustakabali bora kwa sayari yetu, basi unaweza kuwa na kile kinachohitajika kuwa Kijana Bingwa Duniani.

Vigezo vya kuchaguliwa

Katika hatua ya kwanza ya mchakato wa kuchaguliwa, wote waliotuma maombi yatapitiwa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:

  1. P 3 – Athari chanya ambayo wazo lako kuu linaweza kuwa nayo kwa mazingira (sayari (planet)), jamii (watu (peope)) na uwezo wake wa kifedha (mali (prosperity)).
  2. 3 C - Ushahidi kwamba wewe ni mtu anayetamani kujua (curious), mtu jasiri (courageous) na mtu wa kuvutia (colourful).
  3. Kuonyesha kujitolea – Ni muhimu uwe tayari umejaribu kutekeleza wazo lako kuu kwa angalau miezi sita na unaweza kuelezea mafanikio na maendeleo kufikia sasa.
  4. Kupendekezwa - Nguvu za anayekupendekeza.

 

Explore More