11 Aug 2020 Tukio Kushughulikia Mazingira

Kuimarisha miongozo kuhusu lishe ili kulisha watu huku tukijali mazingira katika siku zijazo.

Mapendekezo mengi kuhusu lishe yanayotolewa na serikali za kitaifa hayaingiani na malengo ya kimataifa kuhusu mazingira na afya kama vile Mkataba wa Hali ya Hewa wa Paris na Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Haya ni matokeo ya utafiti wa kwanza kufanyika ili kuchangunua matokeo kwa afya na mazingira kutokana na miongozo ya kitaifa ya lishe katika nchi 85 ulimwenguni.

“Mifumo ya chakula ina madhara makubwa kwa mazingira, na bila kubadilisha mienendo ya chakula na kula zaidi chakula kutoka kwa mimea, kutakuwa na madhara makuu kwa mazingira kutokana na mabadiliko ya tabianchi, matumizi ya ardhi, uchotaji wa maji safi na kemikali zinazotokana na matumizi ya mbolea," ulionyesha utafiti uliofanywa na vyuo vikuu vya Oxford, Harvard, Tufts na Adelaide, uliochaposhwa Julai, 2020.

Pia, ulibainisha kuwa asilimia 98 ya miongozo ya kitaifa hayaendi sambamba na malengo ya kimataifa kuhusu mazingira na afya. Hii inamaanisha kuwa hata kama wangeifuata kote duniani, bado hatungefaulu kufikia malengo yaliyowekwa na serikali.

Kwa kutoa ushauri wa wazi kuhusu  kudhibiti, mara nyingi, vyakula kutoka kwa wanyama - hasa, nyama na maziwa - vina uwezekano mkubwa wa kuimarisha miongozo kuhusu lishe na kuwa na mazingira endelevu.

"Lishe... lililo na matunda machache na nyama kutoka kwa mifugo na nyama ya mikebe... ni changamoto kubwa mno duniani na katika maeneo mengi, na magonjwa mabaya yanayotokana na lishe mbaya kama vile magonjwa ya moyo, saratani, kisukari (type 2 diabetes), ni ghali mno kuyatibu," utafiti huo ulionyesha.

Madhara kutokana na ongezeko la joto duniani ni makuu: Kilimo husababisha taktibani robo moja ya gesi ya ukaa duniani. Tishio kuu ni ongezeko la mapato duniani—haswa kabla ya janga la korona—yalisababisha ongezeko la nyama na bidhaa kutoka kwa maziwa, chanzo kikubwa cha uzalishaji wa kaboniksidi na methani.

Kupunguza ulaji wa wanyama na ulaji wa kupindukia wa bidhaa kutoka kwa wanyama katika nchi zilizoendelea na kurahisisha upatikanaji wa lishe katika nchi maskini kunaweza kuimarisha matumizi ya ardhi, kupunguza bei ya lishe bora kote duniani na kupunguza uzalishaji wa gesi chafu.

“Inaashiria kuwa mwanya kati ya uzalishaji halisi wa kaboniksidi na upunguzaji wake tunaohitaji ili kukaribia nyuzijoto 1.5 unaongezeka,” anasema mtaalamu wa hali ya hewa na Shirika la Mazingira Duniani (UNEP), Niklas Hagelberg.

"Tunachokula, na mapendekezo ya serikali ya kitaifa kuhusu jinsi tunavyopaswa kubadilisha mienendo yetu ya ulaji vinaweza kuchangia pakubwa katika upunguzaji wa uzalishaji wa gesi ya ukaa. Ila mapendekezo na sheria havitoshi. Sera za kudumu zinazoeleweka kwa urahisi zinahitajika ili kuhakikisha kuwa zinaenda sambamba na sera za nchi za kilimo na kuhakikisha kuwa watu wanazifuata."

 

Mnamo tarehe 1 Septemba, UNEP na Mfuko wa Wanyamapori Duniani watachapisha makala na kichwa cha Kuimarisha Michango Inayowekwa na Taifa kwa Mifumo ya Chakula: Mapendekezo kwa WafanyaMaamuzi.

Ripoti ya mwaka wa 2019 ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula (FAO) ilionyesha kuwa nchi zikitekeleza ahadi zake za kubadilisha mifumo ya chakula na kukuza kilimo endelevu ni muhimu katika kukabiliana na baa la njaa na utapiamlo kufikia mwaka wa 2030. FAO ilipendekeza matumizi ya njia jumuishi inayokata katika sekta mbalimbali ili kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa na kujiimarisha.

  

Kwa taarifa zaidi, tafadhali walisiana na Niklas Hagelberg: Niklas.hagelberg@un.org