Je, unatafuta njia rahisi zitakazokuwezesha kuchukua hatua zinazoweza kutekelezeka ili kupunguza uchafuzi unaotokana na gesi ya ukaa na hata kushawishi wenzako kufanya hivyo? Hapa kuna hatua 16:
Hatua hizi zinazotolewa na wataalamu na kutoka kwa utafiti wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na utafiti mwingineo, zimejumuisha kwenye kampeni ya Count Us In, kampeni inayoleta pamoja tamaduni mbalimbali, dini mbalimbali, spoti mbalimbali na mashirika mbalimbali ya biashiara.
Waandaaji wake wanatarajia kuwa shughuli na msaada waliopata kutoka kwa wabia utashawishi watu bilioni moja kuchukua chukua hatua kwa vitendo ili kupunguza uchafuzi unaotokana na gesi ya ukaa na kutoa shinikizo kwa viongozi kushughulikia mazingira ipasavyo.
Juhudi za kila mtu binafsi zinaweza kuwa na athari kubwa. Waandaaji wa Count Us In wanakadiria kuwa iwapo watu bilioni moja watachukua hatua kwa vitendo katika maisha yao, wanaweza kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa duniani kwa asilimia 20.
"Tunakumbwa na majanga matatu duniani kwa sasa- janga la mabadiliko ya tabianchi, janga la mazingira na janga la uchafuzi na taka. Majanga yanayosababishwa na njia mbaya za uzalishaji na utumiaji wa bidhaa, majanga haya matatu yanaharibu mifumo halisi inayowezesha uchumi kustawi. Katika muongo huu tunapoangalia jinsi ya kuishi duniani, ni sharti watu wengi iwezekanavyo wachukue hatua ambazo hawajawahi kuchukua. Juhudi za mtu binafsi ni muhimu na ni sharti zithaminiwe," alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP.
Fuatilia athari zinazotokana na uamuzi wako
Iwapo utajisajili kwenye jukwaa la Count Us In au kupitia kwa majukwa mengine tunayoshirikiana nayo kama vile kampeni ya Umoja wa Mataifa ya #ActNow campaign, unaweza fuatilia hatua zako kwa kushirikiana na mimilioni ya watu.
Ushauri unaotolewa kila siku na mfumo utakaotumia kufuatilia mwenendo wako vinapatikana mtandaoni kwenye apu mpya ya #ActNow kutoka kwa AWorld. Anzisha safari yako endelevu hapa:
Count Us In ilizinduliwa na TED Countdown, mradi wa kimataifa unaoendeshwa na TED na Future Stewards ili kutoa uhamasishaji utaowezesha kupata suluhu kwa changamoto za mazingira.
Shughuli sambamba: TEDxUNEP: Racing to Zero with Higher Education
UNEP na udharura wa kushughulikia mazingira
Ijapokuwa kwa sasa kuna viwango vya juu vya uhamasishaji kuhusu mabadiliko ya tabianchi, bado kuna hali ya sintofahamu na taarifa za kupotosha kuhusu hatua zinazohitajika na uenezaji wa taarifa potovu kuwa kushughulikia mazingira kutaathiri maisha ya binadamu vidaya..
UNEP iko mstari mbele kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Kazi yake inajumuisha sekta za sayansi, sera, teknolojia na fedha. Shirika hili hushirikiana na nchi ili kupunguza uzalishaji wa gesi chafu wakati wa mchakato wa maendeleo na kuimarisha uwezo wa mataifa hayo wa kukabiliana na ongezeko la joto kupitia nature-based solutions.