01 March 2024 Ripoti

Mtazamo wa Rasilimali Ulimwenguni Mwaka wa 2024

Waandishi: UNEP, International Resource Panel (IRP)
Cover

Ulimwengu unakabiliwa na changamoto za aina tatu duniani za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai, na uchafuzi na taka. Uchumi duniani unatumia malighafi nyingi zaidi kuliko wakati mwingine wowote, ili hali ulimwengu hauelekei kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Jamii ya wanasayansi haijawahi kupatana zaidi au kukubaliana zaidi kuhusu hitaji la mabadiliko ya kimataifa ya dharura ya kuwezesha matumizi endelevu ya rasilimali. Toleo hili la mwaka wa 2024 la Mtazamo wa Rasilimali Ulimwenguni linaonyesha umuhimu wa rasilimali kwa utekelezaji bora wa Ajenda 2030 na makubaliano ya kimataifa ya mazingira ya kukabiliana na changamoto za aina tatu duniani.  Ripoti hii inaleta pamoja data bora zaidi iliopo, uwakilishaji na tathmini ili kuchanganua mienendo, athari kwa ujumla na athari kuzingatia makundi mbalimbali. Inaundwa kutokana na kazi ya zaidi ya miaka 15 ya kazi ya Jopo la Kimataifa la Ralimali, ikijumuisha tathmini za kisayansi na maoni kutoka kwa nchi, mtandao mkubwa wa washikadau katika nyanja hii na wataalam wa kikanda.

Ripoti hii inaonyesha jinsi, tangu toleo la mwaka wa 2019 la ripoti hii, mwenendo wa matumizi ya rasilimali duniani umeendelea kuongezeka au kuharakishwa. Ripoti hi pia inaonyesha jinsi mahitaji ya rasilimali yanavyotarajiwa kuendelea kuongezeka katika miongo ijayo. Hii ina maana kwamba, bila hatua za dharura na za pamoja, kufikia mwaka wa 2060 uchimbaji wa rasilimali unaweza kuongezeka kwa asilimia 60 kwa kuzingatia viwango vya mwaka wa 2020 – na kusababisha kuongezeka kwa uharibifu na vitishio.

Hata hivyo, mambo hayapaswi kusalia hivi.  Ripoti hii pia inaelezea uwezekano wa kugeuza mienendo mibovu na kuwezesha binadamu kuanza kuishi kwa njia endelevu.  

Kwa hivyo, hatua thabiti za kisera ni muhimu ili kuachana na shughuli zisizo endelevu, kuharakisha njia za kuwajibika na bunifu za kukidhi mahitaji ya binadamu na kuunda hali mwafaka inayokubalika kwa jamii na usawa katika mabadiliko muhimu. Hii ni pamoja na hatua za haraka za kujumuisha rasilimali katika uwasilishaji wa mikataba ya kimataifa ya mazingira, kuweka njia za matumizi endelevu ya rasilimali na kuzindua mipango mwafaka ya kutia motisha ya kifedha, kibiashara na kiuchumi. Uwezekano wa kufikia uendelevu unazidi kuwa finyu na kukabiliwa na changamoto, na fursa iliopo inadidimia.  Sayansi iko wazi:  Swali kuu sio tena ikiwa mabadiliko ya utumiaji na uzalishaji wa rasilimali kwa njia endelevu ni muhimu, lakini jinsi ya kufanya hili lijiri sasa.  Kushughulikia ukweli huu, kwa msingi wa dhana zinazobadilika za mabadiliko ya haki, ni sehemu muhimu ya mbinu yoyote inayoaminika na inayokubalika ya kutuwezesha kusonga mbele.

Kuangazia Ripoti ya Mtazamo wa Rasilimali Ulimwenguni ya Mwaka wa2024

Nairobi, Machi 1, 2024 – Uchimbaji wa malighafi Duniani uliongezeka mara tatu zaidi katika miongo mitano iliyopita, inahusiana na ujenzi mkubwa wa miundomsingi katika sehemu nyingi duniani na viwango vya juu vya matumizi ya nyenzo, hasa katika nchi za kipato cha kati za juu  na nchi za kipato cha juu.

Global Resources Outlook press statement by UNEP Executive Director

UNEP Executive Director, Inger Andersen, speaks at the launch of Global Resources Outlook 2024, highlighting the urgent need to address the triple planetary crisis through sustainable resource management and circular economy models. She emphasizes the benefits of decoupling economic growth from resource use and environmental impacts. The report outlines actionable steps for achieving…

Rich countries use six times more resources, generate 10 times the climate impacts than low-income ones

Nairobi, 1 March 2024 – Extraction of the Earth’s natural resources tripled in the past five decades, related to the massive build-up of infrastructure in many parts of the world and the high levels of material consumption, especially in upper-middle and high-income countries. Material extraction is expected to rise by 60 per cent by 2060 and could derail efforts to achieve not only…