Report

Uchunguzi wa Jinsi Beijing Imekabiliana na Uchafuzi wa Hewa kwa Kipindi cha Miaka 20

29 June 2019

Katika mwaka wa 1998, Beijing ilianzisha programu kuu ya kudhibiti uchafuzi wa hewa, na kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita jiji limeweka mikati kadhaa ikiwa ni pamoja na kuweka miundo mbinu mwafaka kabisa za nishati, kudhibiti uchafu unaotokana na matumizi ya makaa ya mawe na kudhibiti kiwango cha moshi unaotolewa na magari. Juhudi hizi zilifaulu kupunguza uchafuzi wa hewa. Kwa miaka mitano kati ya 2013 na 2017, uchafuzi unaotokana na chembechembe ndogondogo (PM2.5) ulipungua kwa asili mia 35 huko Beijing na kwa asili mia 25 kwa maeneo yaliyo karibu. Ripoti hii inaonyesha jinsi ambavyo programu ya Beijing ya kutunza hewa imebadilika katika kipindi cha robo ya karne na kutoa mapendekezo kwa hatua za karibu, za baadaye na hatua za mda mrefu zilizoweza kuchukuliwa na Beijing ili kudumisha azimio lake la kuwa na hewa safi. Mafundisho, sera na yalitokea kwenye ripoti hii yanaweza kusaidia kufikia uamuzi wa jinsi ya kupunguza uchafuzi wa hewa katika miji mingine inayotaka kuboresha hewa.

 

Mada