Kesi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ni suluhisho la kimataifa la kubadilisha mienendo ya mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Ripoti hii ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi Duniani: Uchanganuzi wa Hali Mwaka inaonyesha kuwa idadi ya watu wanaoenda mahakamani kukabiliana na janga la mabadiliko ya taianchi inaongezeka. Kufikia Desemba mwaka wa 2022, kumekuwa na kesi 2,180 zinazohusiana na mazingira zilizowasilishwa kwa taasisi za sheria 65 kote duniani: ikijumuisha mahakama ya kimataifa na kikanda, mabaraza ya hukumu, mashirika ya kimahakama, na taasisi nyingine zinazotoa hukumu ikijumuisha Taratibu Maalum za Umoja wa Mataifa na mahakama za upatanisho. Hii inawakilisha ongezeko kubwa kutoka kesi 884 katika mwaka wa 2017 na kesi 1,550 katika mwaka wa 2020. Watoto na vijana, makundi ya wanawake, jamii za wenyeji, na Watu wa Kiasili, miongoni mwa wengineo, wanatekeleza wajibu mkuu kupeleka kesi hizi mahakamani na kupigania mabadiliko katika ushughulikiaji wa mabadiliko ya tabianchi katika nchi zaidi na zaidi kote ulimwenguni.
Ripoti hii, ambayo ni masasisho ya ripoti za awali za Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa zilizochapishwa katika mwaka wa 2017 na mwaka wa 2020, inaangazia kwa ujumla hali ya sasa ya kesi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na masasisho kuhusu mienendo kuhusiana na kesi za mabadiliko ya tabianchi duniani. Inawapa majaji, wanasheria, mawakili, watungasera, watafiti, watetezi wa mazingira, wanaharakati wa mazingira, wanaharakati wa haki za binadamu (ikiwa ni pamoja na wanaharakati wa haki za wanawake), mashirika yasiyo ya serikali, mashirika ya biashara na jamii ya kimataifa kwa ujumla na nyenzo muhimu kuelewa hali ya sasa ya kesi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi duniani , ikijumuisha maelezo ya masuala nyeti ambayo mahakama zimekabiliana nayo wakati wa kushughulikia kesi za mabadiliko ya tabianchi.
Ripoti hii pia inaonyesha umuhimu wa sheria za mazingira katika kukabiliana na changamoto za aina tatu duniani za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai and uchafuzi. Upatikanaji wa haki huwezesha kutunza sheria za mazingira na haki za binadamu na kuwajibisha sekta za umma. Ripoti hii ilizinduliwa sambamba na maadhimisho ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ya kutambua haki ya binadamu ya kuwa na mazingira safi, bora na endelevu (A/RES/76/300), huku kesi nyingi zinazofikishwa mahakamani zikionyesha uhusiano thabiti kati ya haki za binadamu na mabadiliko ya tabianchi. Azimio la UNGA, linalotambua kuwa athari za mabadiliko ya tabianchi zina athari mbaya kwa ufurahiajiwa haki zote za binadamu, huenda likachochea hatua zaidi za kushughulikia mabadiliko ya tabianchi katika siku zijazo.
Machapisho yanayohusiana
Sheria za Mazingira: Ripoti ya Kwanza ya Kimataifa
Ripoti ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi Duniani: Uchanganuzi wa Hali Mwaka wa 2020
Kesi za Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi: Uchanganuzi wa Kimataifa