Katika eneo lote la Ulaya, changamoto kwa mazingira zimewanda kote. Ni pamoja na jinsi ya kutumia rasilimali za mazingira zinazovuka mipaka ya nchi mbalimbali kama vile Bahari Kaspian, kuimarisha rasilimali katika miji, na kukabialiana na athari za mabadiliko ya tabia nchi katika Milima Karpathian.
Tunakabiliana na changamoto hizi na zinginezo kupitia kazi yetu katika maeneo saba ya kimsingi: mabadiliko ya tabia nchi, majanga na mizozo, ushughulikiaji wa mifumo ya ekolojia, usimamizi wa mazingira, kemikali na taka, matumizi mazuri ya rasilimali, na uchunguzi wa mazingira.
Jinsi inavyojitokeza katika Malengo ya Maendeleo Endelevu, mazingira yanaanza kutiliwa maanani wakati wa kufanya maamuzi yoyote. Tunaona chumi zisizochafua mazingira hazipuuzwi kama kawaida. Kwa ushirikiano na wabia wetu, tunatazamia kuendelea kuimarisha hali ya maisha bila kuathiri yale ya vizazi vijavyo.
Sisi ni shirika linalofanya kazi ya mazingira bila upendeleo katika bara la Ulaya. Kwa kuwa kote ulimwenguni, pia tunafanya kazi kuhakikisha kuna sera zitakazopelekea kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu.
Tukiweka vitendoni, hii inamaanisha kuwa sisi hushauri na kuelekeza nchi, sekta za kibinafsi na makundi ya uraia katika juhudi zao za kuhakikisha kuwepo kwa uchumi usiobagua na wala usiochafua mazingira. Hili litawezekana kwa kupigia upatu teknolojia ya nishati jadidifu au kuhimiza matumizi ya njia endelevu za usafiri kwa mfano, na kubadilishana mawazo na namna nzuri za kufanya kazi kuhusiana na mada mbalimbali kama vile kilimo endelevu na utumiaji na uzalishaji endelevu.
Huwa tunafanya kazi hii kwa ushirikiano na Washikadau na Vikundi Vikuu 9 - vinavyojumuisha wanawake, wakulima, biashara na viwanda na mashirika yasiokuwa ya Serikali - kuhakikisha kuwa makubaliano, utafiti na vifaa vya maendeleo endelevu vinazingatia maoni yao na kuwa wote wananufaika.
Mtandao wa Mazingira wa Geneva (GEN) ni muhimu mno kwa kazi yetu. GEN inashirikisha zaidi ya mashirika 75, ikiwa ni pamoja na Afisi na miradi ya UN, NGO's, taasisi za elimu na serikali za mitaa. GEN ina makao yake Geneva na hujshughulikia na mazingira na maendeleo endelevu. Tangu mwaka wa 1999, Sekretarieti ya GEN - ikiongozwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Maataifa na kwa ufadhili kutoka kwa Afisi ya Mazingira ya Uswizi- imeimarisha ushirikiano na ushirika kati ya washirika wake kupitia uandaaji na mazungumzo mbalimbali na hafla zinginezo. Mtandao huu ni rasilimali kwa sekta yoyote inayotaka kujifundisha juu ya mazingira, kuwa na uchumi usiochafua mazingira na kuwa na maendeleo endelevu.
Juhudi zetu zimezaa matunda kutokana na wabia wetu wanaotoka katika sekta mbalimbali. Sisi huwategemea wabia wetu zaidi ili kuboresha hali ya maisha ya nchi na watu, sasa na siku zijazo.