• Maelezo ya Jumla
  • UNEP side events

Kila mwaka, Jukwaa la Kisiasa la Kiwango cha Juu kuhusu Maendeleo Endelevu (HLPF) la Umoja wa Mataifa hufanya mkutano ili kuendeleza ajenda ya Mifumo ya Umoja wa Mataifa inayohusu maendeleo endelevu. Huku COVID-19 ikiendelea kuhangaisha dunia, mkutano wa mwaka huu ni muhimu zaidi. Katika hali ya sintofahamu inayoendelea,  HLPF inatoa fursa kwa serikali na mashirika ya uraia kuanza kujadiliana kuhusu jinsi watakavyoshirikiana kujiimarisha vyema bila ubaguzi na kuwa dhabiti baada ya korona.

Kwa mara ya kwanza, mkutano wa kila mwaka wa HLPF utafanyika mtandaoni na kuleta pamoja wawakilishi kutoka nchi zote zilizo wanachama wa Umoja wa Mataifa, pamoja na makundi ya mashirika ya uraia. Kwa zaidi ya siku kumi, watatathmini hatua zilizopigwa ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na kujadiliana kuhusu umuhimu wa kutumia mbinu itakayoshirikisha mataifa mbalimbali ili "kujiimarisha" baada ya korona. UNEP itakuwepo ili kuongoza majadiliano kuhusu umuhimu wa kushughulikia masuala ya mazingira kwa dharura, kupitia shughuli zinginezo tano zitakazoendeshwa mkutano huu utakapokuwa unaendelea. Shughuli hizo za pembeni zitaangazia jinsi ya kubadilisha uchumi wa kimataifa na kuufanya kutochafua mazingira, ulio na usawa na dhabiti bila kubagua.

Soma zaidi