• Maelezo ya Jumla

Nini: Kikao cha tano cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa kitaimarisha juhudi za kushughulikia mazingira kweye muktadha wa maendeleo endelevu, na kutoa kipaumbele kwa utekelezaji wake kikamilifu. Kikao hiki cha tano cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa katika mwaka wa 2021 kitatumiwa kuhamasisha, kutia motisha na kutia moyo Nchi Wanachama na wadau kushiriki na kutekeleza mbinu mwafaka na masuluhisho yanayotokana na mazingira yatakayochangia kufikia Ajenda 2030 na Malengo ya Maendeleo Endelevu, hasa kutokomeza umaskini na kubuni ruwaza endelevu ya uzalishaji na matumizi ya bidhaa.

Kaulimbiu: Kuimarisha Juhudi za Kushughulikia Mazingira ili Kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu

Kaulimbiu hii kwa hivyo inatoa wito wa kuimarisha juhudi za kushughulikia na kuboresha mazingira na kutoa masuluhisho yanayotokana na mazingira ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu kupitia vipengele vyake vitatu vinavyoingiliana vya (kijamii, uchumi na mazingira).  

Kaulimbiu mbiu hii ilikubaliwa wakati wa mkutano uliojumuisha Baraza la Utawala na Kamati ya Mabalozi wa Kudumu uliojiri tarehe 3 Disemba mwaka wa 2019, baada ya majadiliano ya kina na Nchi Wanachama na wadau wakiongozwa na Bw. Fernando Coimbra, Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa Kudumu, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Brazil nchini Kenya, na Bi. Elin Bergithe Rognlie, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Norway nchini Kenya.

Rais wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa ataendelea na majadiliano kuhusiana na maandalizi ya kikao cha tano cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa ili kuhakikisha kuwa mkutano wa mwka wa 2021 utafaulu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Secritarieti ya UNEP kupitia unep-sgb@un.org

Lini: Februari 22 hadi 26, 2021

Wapi: Nairobi, Kenya

Pata maelezo zaidi hapa.