• Maelezo ya Jumla
  • Ratiba
  • Makala ya Kutumiwa
  • Hotuba
  • Rasilimali zaidi

Lini: Machi 3 - 4, 2022

Wapi: Nairobi, Kenya

Kikao cha tano cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa kilifuatiwa na kikao maalum kinachotambulika kana UNEP@50, kilichoendeshwa Machi 3 - 4, 2022, ili kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP). Kikao hicho maalum kiliendeshwa chini ya kaulimbiu ya "Kuimarisha UNEP ili kutekeleza kipengele cha mazingira cha Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu."

UNEP@50 umekuwa wakati wa kutafakari kuhusu yaliyopita na kutazamia yajayo. Ilitoa fursa ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kuchochea hatua za pamoja za kushughulikia changamoto tatu duniani za mabadiliko ya tabianchi, uharibufu wa mazingira na bayoanuai, na uchafuzi na taka. Hakuna nchi au bara linaloweza kutatua changamoto hizi za kimataifa bila kusaidiwa.  Lakini kila taifa lina wajibu muhimu wa kutekeleza kulinda watu wetu na sayari yetu.

Azimio la kisiasa lililopitishwa tarehe tatu 3 Machi, 2022 wakati wa kikao maalum cha UNEA kuhusu UNEP@50

Tafadhali pokea makala mwafaka na ratiba ya maadhimisho haya kwenye tabu zilizopo hapo juu

Kikao cha tano cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA-5.2) kiliendesha mtandaoni na mjini Nairobi, Kenya, kuanzia tarehe 28 Februari hadi tarehe 2 Machi mwaka wa 2022. Punde tu baada ya UNEA-5.2, Kikao Maalum cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa kiliendeshwa tarehe 3 na 4 Machi mwaka wa 2022, kilichotengewa maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa  katika mwaka wa 1972 (UNEP@50).

Hafla za kando wakati wa UNEA-5 ziliangazia “Kuimarisha juhudi za kushughulikia mazingira ili kufikia malengo ya Maendeleo Endelevu" na maadhimisho ya Miaka 50 ya UNEP.

Tazama kalenda inayoingiliana na upeperushaji wa moja kwa moja hapa 

Tazama Kikao Maalum cha maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa(UNEP@50)

 

Ajenda ya kwanza: Kikao cha ufunguzi

Ajenda ya pili: Kuidhinishwa kwa agenda na ratiba ya shughuli

Ajenda ua mda iliyofafanuliwa  Kiingereza | Kiarabu | Kichina | Kifaransa | Kirusi | Kihispania Ilipakiwa Februari 14, 2022

Ratiba ya kazi Ilipakiwa Februari 14, 2022

Makala kuhusu hali ya UNEA 5.2 na UNEP@50 Ilipakiwa Februari 15, 2022

Ajenda ya tatu: Wasifu wa wawakilishi

Ujumbe wa mwisho kutolewa na Mkurugenzi Mtendaji Ilipakiwa Februari 14, 2022

Ajenda ya nne: Hotuba kutoka kwa wawakilishi

Iliyopitiwa - Maelekezo kuhusu utoaji wa hotuba na nchi na washikadau wakati wa kikao maalum cha maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa UNEP Ilipakiwa Februari 14, 2022

Ajenda ya tano: Uwasilishi wa ripoti na Mkurugenzi Mtendaji kuhusu uhusiano wa sera na sayansi

Hatua za utelezaji wa azimio 4/23 kuhusu kukuza uhusiano kati ya sera na sayansi ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa:    Kiingereza | Kiarabu | Kichina | Kifaransa | Kihispania | Kirusi  Ilipakiwa Februari 14, 2022

Toleo la ripoti "Kutafakari kuhusu yaliyopita na kuwazia siku zijazo: mchango wa mazungumzo kuhusu uhusiano wa sera na sayansi":  Kiingereza | Kiarabu |  Kichina | Kifaransa Kihispania | Kirusi  Ilipakiwa Februari 15, 2022

Ajenda ya sita:  Wasilisho la ripoti ya washikadau inayojulikana kama "UNEP Tunayoitaka"

Tamko la Pamoja Lililotolewa na Makundi Makuu na Washikadau kote Duniani Ilipakiwa Februari 21, 2022

Wasilisho la ripoti ya washikadau inayojulikana kama "UNEP Tunayoitaka" Ilipakiwa Februari 23, 2022

Ajenda ya saba: Majadilialo ya viongozi

Kikao maalum cha maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP@50)- Makala la Majadiliano ya Ngazi ya Juu Ilipakiwa Februari 14, 2022

Maelekezo kuhusu kushiriki kwa majadiliano ya viongozi Ilipakiwa Februari 14, 2022

Ajenda ya nane: Majadilialo ya washikadau anuai

Kikao maalum cha maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP@50)- Makala ya Majadiliano ya Ngazi ya Juu ya Washikadau Anuai Ilipakiwa Februari 14, 2022

Maelekezo kuhusu kushiriki kwa majadiliano ya ngazi ya juu ya washikadau anuai Ilipakiwa Februari 14, 2022

Ajenda ya tisa: Kukubali matokeo ya kisiasa ya kikao

Utekelezaji wa Azimio la Baraza 73/333, linalojulikana kama “Ufuatiliaji wa Ripoti wa Kikundi Kazi Wazi cha Mda Kilichoanzishwa kwa Kuzingatia Azimio la Baraza 72/277”

Ajenda ya kumi: Kupitishwa kwa ripoti ya kikao na muhtasari wa Mwenyekiti

Ajenda ya kumi na moja: Kuhitimisha kikao

Rasimu ya majadiliano ya Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa la katika kikao chake maalum cha kwanza: maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa Ilipakiwa Februari 14, 2022

  •