23 Jun 2019 Toleo la habari Kutumia mazingira kushughulikia tabianchi

Mkutano Mkuu wa Uchumi utokanao na Wanyama Pori kuzindua dira ya Uhifadhi inayoongozwa na Waafrika

Nairobi/Victoria Falls, 23 Juni 2019 - Wakuu wa nchi, viongozi wa biashara, wataalamu wa kiufundi na wawakilishi wa jamii watakusanyika Zimbabwe katika mji wa Victoria Falls kutoka tarehe 23-25 Juni kwa Mkutano Mkuu wa Uchumi utokanao na Wanyama Pori (the Africa Wildlife Economy Summit), kwa nia ya kubadilisha jinsi uchumi wa kiasili unavyoendeshwa.

Mkutano uliandaliwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na Umoja wa Afrika (AU) na mwenyeji wake ni Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa, Rais wa Zimbabwe, huo Mkutano Mkuu utazindua Mradi wa Kiafrika wa Uchumi utokonao na Wanyama Pori- dira mpya, ya uhifadhi inaongozwa na Waafrika inayounganisha sekta za kibinafsi na mashirika ya kitaifa na wanakijiji ili waanzishe na kufadhili miradi inalenga kuhifadhi mazingira na kusabisha uchumi endelevu na kutoa makufaa ya kiekolojia kwa nchi, watu na kwa mazingira.

Angalau mawaziri 12 kutoka Angola, Zimbabwe, Botswana, Gambia, Zambia, Chad, Sudan Kusini wananuia kuhudhuria, pamoja na wawekezaji wa kibinafsi katika sekta za utalii na uhifadhi, wawakilishi kutoka vijijini, wanasanyansi wanaojishughulisha na uhifadhi na waunda sera. Wawakilishi wanatarajiwa kutoka katika takribank mataifa 30.

Biashara vinavyoendeshwa kutokana na mali asili na wanyama pori - ikiwa ni pamoja na utalii, uvunaji wa mimea na vitu vya asili ili kutumia kama chakula, vipodoshi au madawa, miradi ya kutoza ushuru kwa ajili ya kuhifadhi wanyama pori, au ada, ushuru na kodi ambazo hutozwa kutokana na matumizi ya mali asili na kadhalika - huajiri mamilioni ya watu ya kuzipa serikali mapato ya mamilioni ya dola. Kando na manufaa kwa biashara, uhifadhi wa mazingira una manufaa kwa wanakijiji, kwa maeneo na kwa dunia nzima.

Toleo la 'A Working Paper by Space for Giants', kwa ufadhili wa UNEP na Kituo Kinachofuatilia Uhifadhi Duniani cha World Conservation Monitoring Center - litazinduliwa kwenye mkutano huo - linaonyesha kuwa matumizi ya pesa kwa utalii, taasis za burudani na mapumziko barani Afrika ni takribani dola bilioni 124 mwaka wa 2015, na zinatarajiwa kufika dola bilioni kufikia mwaka 2030. Ijapokumi kuwa chumi zinazotegemea wanyama pori zinaendelea kukua, ni sharti zisingatie ukuaji wa kiuchumi, kijamii na wa kiekolojia.

Muhimu ili kukuza jamii ni kuhakikisha ya kwamba wanajamii ni washika dau wenza katika uchumi unaotegemea mali asili. Watu wanaoishi na mali asili sharti wawe nguzo ya yanayojiri, na jamii zinapaswa kuchukuliwa kama wabia wenza, wakiwa na matamanio yao binafsi ya kuhifadhi na ya maendeleo yanayothaminiwa wakati wa kuhifadhi spishi.

"Ili kuokoa wanyama pori na kutunza vipato, ni sharti tuhakishe ya kuwa maeneo ya wanyama pori yasalie halali na yanayoweza kutumiwa vizuri," alisema Joyce Msuya, Naibu wa Mkurukenzi Mtendaji wa UNEP. "Ni sharti tubuni uchumi mpya unaofanya kazi vizuri unaotegemea wanyama pori."

"Afrika imepiga hatua kwa kuhifadhi maeneo asili na kuhifadhi wanyama pori na mifumo ya ekolojia," alisema mheshimiwa Balozi Josefa Correia Sacko, Kamishna wa AU wa Uchumi wa Vijijini na Kilimo (AU Commissioner for Rural Economy and Agriculture.) "Wakati umetimia wa kuimarisha uchumi kupitia ubia unaojumuisha sekta za umma na za kibinafsi unaongozwa na Wafrika na ambao unashirikisha jamii kama nguzo katika uwekezaji, huku ukiwajibikia hoja ya kuendelea kuhifadhi.

Kujitolea kwa dhati na miradi mipya inatarajiwa kuibuka kutokana na mkutano mkuu, pamoja na warsha na makongamano yatakayofuatia.

 

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa 

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa ndilo sauti kuu ya kimataifa kuhusu mazingira. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika kutunza mazingira kupitia kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo. Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa hufanya kazi pamoja na serikali, sekta ya kibinafsi, mashirika ya uraia na Taasis zinginezo za Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa kote ulimwenguni.

 

Mkutano Mkuu wa Uchumi utokanao na Wanyama Pori

Mkutano umeandaliwa na UNEP na Umoja wa Afrika kwa ushirikiano kutoka kwa Space for Giants, Mfuko wa Wanyama Pori Duniani (World Wildlife Fund), UNDP, Muungano wa Ulaya, na wengineo.

Kwa taarifa zaidi

Keishamaza Rukikaire, Mkuu wa Habari na Vyombo vya Habari, UNEP +254722677747