Pixabay
10 Mar 2021 Toleo la habari Uchumi usiochafua mazingira

Je, tunapiga hatua mwafaka ili kujiimarisha baada ya korona bila kuchafua mazingira? Bado

Oxford/Nairobi, Machi 10, 2021 – Mwaka mmoja tangu janga la korona lilipoanza, matumizi ya fedha za kujiamarisha baada ya korona haijaendana na ahadi zilizotolewa na mataifa za kujiimarisha kwa njia endelevu. Uchanganuzi wa matumizi ya fedha ya nchi za chumi kuu, ulioendesha na mradi wa Oxford- kwa ushirikiano na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), unaonyesha kuwa ni asilimia 18 tu ya fedha zilizotengewa kuimarisha uchumi baada ya korona zinaweza kutumika bila uchafuzi wa mazingira.

Ripoti hiyo, Je,Tunajiimarisha Bila Kuchafua Mazingira? Idhibati kutoka kwa Mwaka wa 2020 na Hatua za Kutumia Fedha za Kujimairisha Baada ya korona Bila Kuchafua Mazingira , ni wito kwa serikali kuwekeza kwa njia endelevu zaidi na kukabiliana na ukosefu wa usawa huku huku zikifanya maendeleo ili kukabiliana na madhara mabaya ya janga la korona.

Uchangunuzi wa kina mno wa bajeti ya kukabiliana na mambo yanayohusiana na COVID-19 na juhudi za kujiimarisha baada ya janga za chumi kuu 50 kufikia sasa, ripoti hiyo inaonyesha kuwa ni dola bilioni 368 kati ya dola trilioni 14.6 zilizotengewa COVID (za kunusuru na kuimarisha uchumi) katika mwaka wa 2020 zinazingatia kutochafua mazingira.

Katibu Mtendaji wa UNEP, Inger Andersen: “Binadamu wamekabiliwa na janga, changamoto za kiuchumi na uharibifu wa mifumo ya ekolojia - hatuwezi kubali kushindwa. Serikali zina fursa ya kipekee ya kuanza safari ya kufanya maendeleo kwa njia endelevu inatoa kipaumbele kwa uchumi, kupunguza umaskini na kutunza mazingira - Observatory inazipa vifaa vitakavyoziwezesha kuwa endelevu zaidi na kujiimarisha pasipo na kubagua."

Brian O’Callaghan, mtafiti mkuu kwenye Kuimarisha Uchumi wa Chuo Kikuu cha Oxford na mwandishi wa ripoti: "Licha ya hatua bora za kuwezesha kujiimarisha kwa njia endelevu baada ya COVID-19 kutoka nchi chache kuu, dunia haijaweza kufikia malengo yake ya kujiimarisha vyema baada ya janga. Ila fursa za kutumia fedha vizuri hazijaisha kabisa. Serikali zinaweza kutumia wakati huu kupata ustawi wa muda mrefu wa kiuchumi, kijamii na wa mazingira."

"Uwezo wetu wa kuarifu na kufuatilia vizuri uwekezaji uliofanywa na nchi kukabiliana na athari za COVID-19 kwa jamii na kwa uchumi ni muhimu ili kujiimarisha kwa njia isiyobagua na inayojali mazingira," alisema Achim Steiner, Msimamizi wa UNDP. "Kwa kuzingatia haya, Global Recovery Observatory na UNDP’s Data Futures Futures Platform wanatoa kwa watungasera data na maarifa mpya ya kina, – kuwezesha rasilimali hizi kupatikana kwa urahisi kutasaidia kuimarisha uwazi, uwajibikaji, uwekezaji mwafaka unaofanywa kwa sasa na kuathiri uendelevu wake katika siku zijazo."

Profesa wa Uchumi wa Mazingira katika Chuo Kikuu cha Oxford, Cameron Hepburn: "Ripoti hii inatutaka kuwajibika. Data kutoka kwa Global Recovery Observatory inaonyesha kuwa hatujiimarishi vyema zaidi, kwa sasa. Tunajua kuwa kujiimarisha bila kuchafua mazingira ni muhimu kwa uchumi na mazingira - sasa tunapaswa kuchukua hatua."

Ripoti hiyo inasisitiza kuwa kujiimarisha bila kuchafua mazingira kunaweza kuwa na manufaa makubwa kwa ukuaji wa uchumi, huku kukisaida kufikia malengo ya kimataifa ya mazingira na kupunguza ukosefu wa usawa wa kimuundo. Kukomesha miongo ya umaskini, nchi za kipato cha chini zitahitaji mikopo ya kutosha kutoka kwa wabia wa kimataifa.

Maswali tano yanaibuka kuhusiana na safari ya kujiimarisha kwa njia endelevu:

  • Ni kipi kilicho hatarani wakati ambapo nchi zinatenga rasilimali za kuimarisha uchumi?
  •  Ni matumizi yepi ya fedha yatakayowezesha kuimarisha uchumi na kuwa na mazingira endelevu?
  • Kutumia fedha kuimarisha uchumi kutasaidiaje kukabiliana na ukosefu wa usawa ulioongezeka kutokana na COVID-19?
  • Ni uwekezaji upi wa kiuchumi unaofanywa na nchi kwa sasa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira na uchafuzi?
  • Ni yepi zaidi yanayopaswa kutekelezwa ili kuhakikisha tunajiamarisha kwa njia endelevu isiyobagua?

Kwa jumla, matumizi ya fedha kwa njia inayojali mazingira "hayajakuwa yakiambatana na changamoto zinazoendelea za mazingira," kulingana na ripoti hiyo, ikijumuisha mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira na uchafuzi, na kutofanya jamii kufaidika mno wala kuwa na manufaa ya muda mrefu za kiuchumi.

 

Matokeo makuu ya utafiti huu kwa kuzingatia matumizi ya fedha kuimarisha uchumi:

 

  • Dola bilioni 341 au alimia 18.0 ya fedha zilizotumika ilijali mazingira, na mara nyingi hali hii ilijitokeza kwa nchi chache tu za mapato ya juu. Matumizi ya fedha kuimarisha uchumi baada ya janga la corona yameshindwa kuzingatia uwekezaji usiochafua mazingira.
  • Dola bilioni 66.1 ziliwekezwa kwa nishati iliyo na kiwango kidogo cha gesi ya ukaa, tunapongeza Uhispania na Ujerumani kwa ruzuku kwa miradi ya nishati jadidifu na uwekezaji kwenye haidrojeni na miundo msingi.
  • Dola bilioni 86.1 zilitengewa usafiri usiochafua mazingira kutipia kwa magari ya umeme na ruzuku, uwekezaji kwenye miundo msingi ya usafiri wa umma, baiskeli na kwenda kwa miguu.
  • Dola bilioni 35.2 zilitengewa uimarishaji wa majengo yasiochafua mazingira ili kuimarisha matumizi ya nishati, hasa kupitia kwa kuongeza vitu ambavyo havikuwepo awali, haswa nchini Ufaransa na Uingereza.
  • Dola bilioni 56.3 zilitengewa rasilimali zinazotokana na malighafi au Maluhuhisho Yanatotokana na Mazingira (NbS)– miradi ya kuboresha mifumo ya ekolojia na ya upandaji wa miti. Humusi mbili zilielekezwa kwenye mbuga za umma na mikakati ya kukabiliana na uchafuzi, haswa nchini Marekani, Uchina, na kuimarisha maisha ya watu na kukabiliana na changamoto za mazingira.
  • Dola bilioni 28.9 zilitengewa R&D isiyochafua mazingira. R&D isiyochafua mazingira inajumuisha teknolojia ya nishati jadidifu, teknolojia ya kupunguza gesi ya ukaa katika sekta kama za ndege, plastiki, kilimo na utekaji wa kaboni. Bila kuimarika kwa R&D isiyochafua mazingira, kufikia malengo ya Mkataba wa Paris kutakuwa ghali na kubadili maisha.

MAKALA KWA WAHARIRI

 

  • Global Recovery Observatory ni mradi unasimamiwa na Mradi wa Kuimarisha Uchumi wa Chuo Kikuu cha Oxford (OUERP), kwa ushirikiano na UNEP, Shirika la Fedha Duniani na GIZ kupitia kwa Green Fiscal Policy Network (GFPN). 
  • Kufikia Februari mwaka wa 2021, Observatory ina sera zaidi ya 3,500 kwa nchi 50 za uchumi kubwa zaidi duniani. Husasishwa kila juma. Kihifadhidata chenyewe kitahifadhiwa kwenye Oxford SSEE, GFPN, na kwenye mtandao wa UNDP Data Futures. Pitia kwenye matokeo ya utatiti kwenye jukwaa la UNDP la Data Futures Platform: https://data.undp.org/content/global-recovery-observatory/
  • Makala yanayojumuisha methodojia inayojumuisha mfumo mkuu, mifumo ndogondogo, na tathmini inapatikana kwa O’Callaghan et al., 2020.
  • Masasisho ya hivi karibuni kutoka kwa World Economic Outlook (Januari 2021) yanaonyesha kupungua kwa asimia 3.5 kwa GDP duniani katika mwaka wa 2020 (IMF, 2021).
  • Takwimu zote hapo juu ni Dola za Marekani (USD), kwa kuzingatia ada ya kubadilisha katika mwezi wa Januari mwaka wa 2021.

Chuo Kikuu cha Oxford

Chuo Kikuu cha Oxford kimeorodheshwa kama nambari moja na Times Higher Education World University Rankings kwa mara ya tano mfulilizo, na nguzo ya kufaulu huko ni utafiti wetu wa kipekee na ubunifu. Chuo cha Oxford ni maarufu kwa utafiti wa kipekeee na baadhi ya watu walio na talanta kuu duniani husomea huko. Kazi yetu hunufaisha mamilioni ya watu, wanaotatua matitizo halisi duniani kupitia mtandao mkubwa wa ubia na kushirikiana. Kiwango chake na hali ya kushughulikia taaluma mbalimbali utafiti wetu hupelekea utafiti huchochea kufikiria ubunifu na kutoa masuluhisho.

 

Shule ya Smith ya Biashara na Mazingira

Makao ya Mradi wa Kuimarisha Uchumi wa Chuo Kikuu cha Oxford na Global Recovery Observatory, Shule ya Smith inahudumia taaluma mbalimbali katika Chuo Kikuu cha Oxford. Hujihusisha na ufundishaji, utafiti, kushirikana na mashirika na kampuni za biashara, utunzaji wa kudumu wa mazingira kwa njia endelevu. OUERP ni taasisi duniani ya kuandaa na kupitisha mitazamo ya kiuchumi ya kudumu kuhusiana na matumizi mabaya ya fedha. Shule ya Smith ilianzishwa kupitia ufadhili kutoka kwa Wakfu wa Elimu wa Familia ya Smith na kufunguliwa rasmi katika mwaka wa 2008. www.smithschool.ox.ac.uk

 

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

UNEP in mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.

 

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Sarah Whitebloom, Chuo Kikuu cha Oxford. news.office@admin.ox.ac.uk

Keisha Rukikaire, Msimamizi wa Habari na Vyombo vya Habari, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa rukikaire@un.org, +254 722 677747