11 Dec 2019 Toleo la habari Kushughulikia Mazingira

Kuwajibika ni muhimu ili kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kutoka majumbani na maeneo ya kazi kote ulimwenguni

  • Majengo na ujenzi huzalisha takribani asilimia 40 ya hewa ya kaboniksidi, ila bado hatua zinazochukuliwa hazitoshi.
  • Pamoja na fursa iliopo ya kufikia malengo ya Mkataba wa Paris, sekta hii ni muhimu ili kuwezesha ushughulikiaji mkubwa wa mazingira.

Madrid, Desemba 11, 2019 -- Ni sharti jinzi majengo yanavyojengwa, kutumika na ramali zake duniani kuimarika kwa kasi iwapo sekta kuu ya ujenzi na majengo itashikilia nafasi yake muhimu katika kuafikia malengo ya kimataifa chini ya Mkataba wa Paris.

Ripoti ya kimataifa, iliyotolewa leo wakati wa Kongamano La Kushughulikia Mazingira la Umoja wa Mataifa mjini Madrid, inaonyesha kuwa uchafuzi kutoka kwa majengo na ujenzi bado umeshikilia takribani asilimia 39 ya uzalishaji wa kaboniksidi.

Ripoti hiyo pia inaonyesha mambo ya kutisha – kushinda mambo mazuri yaliyomo — ambayo yanapaswa kushughulikiwa na serikali ili kuweza kufikia malengo ya mwaka wa 2030 na zaidi ya hapo.

Bila kuchukua hatua, mahitaji ya nishati katika sekta hii yanaweza kuongezeka kwa asilimia 50 kufikia mwaka wa 2060, kwa mjibu wa Muungano wa Kimataifa wa Majengo na Ujenzi (GlobalABC)

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa hatuendelei vizuri. Bila kuchukua hatua kali endelevu ongezeko hili la nguvu za umem mahitaji ya nishati kutoka katika sekta hii muhimu inamaanisha hatuwezi kupata mabadiliko yanayohitajika kwa dharura au kufikia malengo ya maendeleo endelevu. 

Uzalishaji wa Gesi Chafu Waongezeka

Uchunguzi wa mwaka uliopita wa 2018 ulionyesha kuwa serikali, mashirika na makampuni yanaendelea vizuri na uzalishaji wa gesi chafu kwa jumla unapungua.

Kuimarika huku kulihusishwa na matumizi mazuri ya nguvu za umeme katika sekta kama vile ya kuleta joto, mwangaza na ya kupika, ikisaidiwa na biashara na majumba yanayotumia nishati isiyochafua mazingira kama vile nishati ya upepo na ya jua.

Lakini ripoti ya leo, iliyotolewa na Shirika la Kimataifa la Nishati  (IEA) na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na, inaonyesha kuwa ijapokuwa uzalishaji wa gesi chafu umeanza kuongezeka tena, juhudi za kukabiliana na uzalishaji wa gesi chafu zinaendelea kuimarika.

Hali hii ni kielelezo cha uzalishaji wa gesi chafu kote ulimwenguni, ulioongezeka katika mwaka wa 2018.

Ongezeko la uzalishaji wa gesi chafu unatokana na hitaji kubwa la matumizi ya nishati, ikiwa ni pamoja na viwanda vinavyotumiwa nishati nyingi kama vile viwanda vya chuma, hali inapelekea matumizi makubwa ya visukuku ili kupata umeme, kwa mfano mawe ya makaa.

Kupungua kwa Uwekezaji katika Matumizi ya Nishati Nzuri

Ripoti ya Hali ya Kimataifa ya mwaka wa 2019, inayotolewa ili kutumiwa na  GlobalABC, pia inaonyesha 'kupungua' na hali inayoendelea kushuhudiwa ya uwekezaji mdogo katika nishati isiyotumia umeme mwingi inahitaji hatua za dharura ili kupunguza uzalishaji wa gesi chafu na kuwezesha kukabiliana na hewa ya ukaa.

Ongezeko la  Vifaa vya Kupunguza Joto katika Maeneo ya Makaazi ni Suala Linalotisha

Ripoti hiyo inaonyesha matokeo chanya katika sekta zingine ikijumuisha matumizi ya taa isiyotumia umeme mwingi kama vile LEDs; madirisha na mifumo ya kupunguza joto iliyoboreshwa; ongezeko la zaidi ya asilimia 20 katika matumizi ya nishati jadidifu ili kuweka mwangaza katika majengo tangu mwaka wa 2010 na kupungua kwa nishati ya kuleta joto.

Hata hivyo, nafasi inayotengewa sakafu imeongezeka kote duniani kwa asilimia 23 tangu mwaka wa 2010, na kwa asilimia tatu tangu mwaka 2017, na matumizi ya umeme katika majengo umeongezeka kwa asilimia saba tangu mwaka wa 2010 na kwa asilimia moja tangu mwaka wa 2017.

Sekta ya kutilia maanani ni kuongezeka kwa 'vifaa vya kupunguza joto' kutokana na ongezeko la wamiliki wa majumba na matumizi ya viyoyozi, ambavyo vimeongezeka zaidi ya mara tatu tangu mwaka wa 2010 na yameongezeka kwa asilimia moja tangu mwaka wa 2017.

Viyoyozi hutumia nguvu za umeme, sanasana kutoka kwa fueli ya visukuku, lakini vina athari za namna mbili, kwa sababu hutumia kemikali za kupunguza joto (CFC and HCFCs), na pia huweza kuzalisha gesi ya ukaa.

  • Juhudi zinafanywa chini ya Mabadiliko yaliyofanyiwa Kigali kwa Mkataba wa Paris  ili kuhamasisha matumizi ya viyoyozi visivyotumia umeme mwingi ambavyo pia hutumia vipunguza joto vilivyo na uwezo mdogo wa kuongeza joto.
  • Kwa kuzingatia kiwango kikubwa cha ongezeko la majengo linaloendelea katika nchi zinazoendelea – wataalamu pia wanasema kuna umuhimu wa kuwa na majengo yaliyo na mifumo ya kupunguzo joto kutegemea eneo la mji. Pia, kuna haja ya kupata suluhu inayozingatia mazingira kama vile kuwa na misitu mijini, mapaa yasiyozalisha gesi ya ukaa na maeneo ya mbele ya nyumba yasiyohitaji mifumo ya kutumia umeme kupunguza joto.

2020: Kila aina ya majengo na ujenzi vizingatiwe katika mikakati ya kitaifa ya kushushughulikia mazingira

Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP, alisema: "Kuna aina mbili kuu ya uhalisia. Kwa kipindi cha miaka 30 ijayo, idadi ya watu duniani ina uwezekano wa kuongezeka kwa bilioni mbili, hali inayoweza kupelekea kuwa na hitaji ya nyumba za makaazi zaidi na ujenzi wa namna hiyo. Kwa wakati uo huo, mataifa yanapaswa kuepukana na hewa ya ukaa iwapo tuna nia ya kuepekana na madhara mabaya ya mabadiliko ya tabianchi".

"Sekta ya majengo na ujenzi ni sharti ikabiliane na hali hii kwa kutoa maeneo ya makazi na ya kufanyia kazi kwa bei nafuu, ya kiwango cha juu, masafi na kamilifi", aliongezea. "Kati ya sasa na mwishoni mwa mwaka wa 2020, kuna fursa kwa serikali kuweka Michango Inayobainishwa na Taifa (NDCs) chini ya Mkataba wa Paris—Ninatoa wito kwa mataifa kuweka sera imara zilizo bayana, kuwekeza na kuchukua hatua zitakazoleta mabadiliko katika majengo na katika ujenzi."

Fatih Birol, Mkurugenzi Mtendaji wa IEA ansema kuwa: "uchanganuzi wetu unaonyesha kuwa kiwango cha uimarishaji wa kawi ulididimia kwa asilimia 1.2 tangu mwaka wa 2017 hadi mwaka wa 2018. Hali hii inahitaji kuimarika kwa asili mia 3 ili kuwezesha kufikia malengo ya Maendeleo Endelevu. Hii ndiyo sababu imetufanya kuunda Kamisheni Kuu ya Kimataifa ili kuchukua Hatua za Dharura katika Matumizi Mazuri ya Nishati ili kupendekeza jinzi ambavyo ukuaji unaweza kuimarishwa kwa kasi kupitia sera mpya imara. Global ABC wamefanya tafiti mbalimbali na kuunda miongozo mbalimbali ya kusaidia serikali na sekta za binafsi kufikia malengo haya ikiwa ni pamoja na Global na Miongozo ya Kikanda kutokomeza uzalishaji wa gesi chafu, kuwa na sekta imara ya majengo na ya ujenzi, na  Mwongozo wa Kujumuisha Utaratibu wa Ujenzi kwenye NDCs

Makala kwa Wahariri

Kuhusu  Muungano wa Kimataifa wa Majengo na Ujenzi (GlobalABC)

GlobalABC ni jukwaa kuu kwa serikali, sekta za kibinafsi, mashirika ya uraia na taasasi kati ya serikali mbalimbali na mashirika ya kimataifa linalotumiwa kuimarisha juhudi za kuhakikisha kuwa hakuna uzalishaji wa gesi chafu, kuna sekta ya majengo na ujenzi inayojitosheleza. Muungano wa Kimataifa wa Majengo na Ujenzi (GlobalABC) ni zao la kongamano la kushughulikia mazingira la UN la mwaka wa 2015.

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

UNEP ni msemaji mkubwa wa kimataifa kuhusu mazingira. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika kutunza mazingira kupitia kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na:

Nick Nuttall, Mshauri wa Mawasiliano COP25, Muungano wa Kimataifa wa Majengo na Ujenzi (GlobalABC)
Keishamaza Rukikaire, Msimamizi wa Habari na Vyombo vya Habari, UNEP +254717080753