PIcha: UNDP/ Shahzad Ahmad
03 Nov 2022 Toleo la habari Kushughulikia Mazingira

Madhara yanapozidi kuwa mabaya kwa kasi, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ni suala linalopaswa kupewa kipaumbele kote ulimwenguni –…

  • Zaidi ya nchi nane kati ya kumi, Wanachama wa UNFCCC, zina chombo cha kuweka mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
  • Makadirio ya gharama za kukabiliana na hali ni mara tano hadi kumi kuliko usambasaji wa kimataifa wa fedha za kukabiliana na hali kwa nchi zinazoendelea 
  • Utashi wa kisiasa ambao haujawahi kushuhudiwa na uwekezaji wa muda mrefu zaidi wa kukabiliana na hali unahitajika kwa haraka

Nairobi, November 3, 2022 – Madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanapozidi kuwa mabaya, Mataifa yanapaswa kuimarisha ufadhili na utekelezaji wa hatua za kusaidia mataifa na jamii zilizo hatarini zaidi kukabiliana na mapigo ya tabianchi, kwa mjibu wa ripoti mpya ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP).

Ripoti iliyozinduliwa leo tunapoelekea COP27 – Mazungumzo yanayoendelea kuhusiana na mazingira mjini Sharm El-Sheikh, nchini Misri – Ripoti ya Kukabiliana na Pengo la Uzalishaji wa Gesi Chafu Mwaka wa 2022: Hatua Ndogo, Mwendo wa Konokono – Kukosa kushughulikia mazingira ni kuhatarisha Dunia, inadokeza kuwa juhudi za kimataifa za upangaji, ufadhili na utekelezaji wa kukabiliana na pengo hazilingani na hatari zinazoongezeka.

"Mahitaji ya kukabiliana na hali katika ulimwengu unaoendelea yanatarajiwa kuongezeka hadi kufikia dola bilioni 340 kwa mwaka kufiki mwaka wa 2030. Hata hivyo ufadhili wa kukabiliana na hali hiyo kwa sasa ni chini ya moja kati ya kumi ya kiasi hicho. Watu na jamii zilizo hatarini zaidi zinalipia gharama ghali. Hali haiwezi kuendelea hivyo," Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alisema katika taarifa yake kuhusu kuzinduliwa kwa Ripoti ya Kukabiliana Na Pengo la Uzalishaji wa Gesi Chafu.

"Kukabiliana na hali ni sharti kushughulikiwe kwa kwa kiwango kinachoonyesha watu wote katika jamii wanathaminiwa kwa njia sawa. Ni wakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi duniani bila kutoa vijisababu na kuwajibika kurekebisha mambo," aliongezea.

Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP, alisema: “Mabadiliko ya tabianchi ni pigo kubwa kwa wanadamu, kama ilivyoshuhudiwa katika mwaka wa 2022: hasa kupitia mafuriko makubwa yaliyoshuhudiwa katika sehemu kubwa ya Pakistan,” alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP. "Dunia inapaswa kusitisha uzalishaji wa gesi ya ukaa kwa dharura ili kudhibiti athari za mabadiliko ya tabianchi. Pia ni sharti tuimarishe kwa dharura juhudi za kukabiliana na athari zilizopo za mabadiliko ya tabianchi na zile zitakazojiri baadaye.

“Mataifa ni lazima yaunge mkono maneno makali katika Mkataba wa Hali ya Hewa wa Glasgow kwa kuchukua hatua dhabiti za kuimarisha uwekezaji wa kukabiliana na hali na kuimarisha matokeo, kuanzia kwa COP27.”

Madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanaongezeka

Ukame wa miaka mingi katika Pembe ya Afrika, mafuriko yasiyotarajiwa Asia Kusini na joto kali la majira ya kiangazi kaskazini mwa dunia ni hatari kwa mazingira. Athari hizi zinatokea kiwango cha nyuzijoto 1.1 tu zaidi ya halijoto ya kabla ya viwanda.

Kwa mjibu wa ripoti ya UNEP ya Pengo la uzalishaji wa Gesi Chafu – iliyochapishwa hivi karibuni na iliyo na uhusiano na Ripoti ya Kukabiliana Na Pengo la Uzalishaji wa Gesi Chafu – Ahadi Zinazotolewa na Taifa (NDCs) chini ya Mkataba wa Paris zinakisia ongezeko la joto duniani litafikia kati ya nyuzijoto 2.4 na 2.6 kufikia mwishoni mwa karne hii. Utafiti wa Jopo la Serikali Mbalimbali Kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (IPCC), unasema kuwa madhara ya mabadiliko ya tabianchi yataongezeka kutokana na kuongezeka kwa kila sehemu ya digrii.  

Hali hii inaonyesha kukabiliana na hali kunapaswa kupewa kipaumbele, ikijumuisha kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi duniani, ripoti inavyoonyesha. Hata hivyo, kwa kuwa uwekezaji kabambe katika kukabiliana na hali hii hauwezi kuzuia kikamilifu athari za mabadiliko ya tabianchi, hasara na uharibifu lazima vishughulikiwe ipasavyo.

Hatua za kukabiliana na hali ni chache na kwa mwendo wa konokono

Zaidi ya nchi nane kati ya kumi sasa zina angalau chombo kimoja cha kupanga mikakati ya kitaifa, na zinaendelea kuwa bora na jumuishi zaidi. Theluthi moja ya Nchi 197 Wanachama wa Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC) wamejumuisha malengo yaliyoainishwa na kuwekewa muda maalum, ambayo ni sehemu inayoongezeka ya mikakati ya ukabilianaji wa kitaifa. Takriban asilimia 90 ya zana za upangaji zilizochanganuliwa zilijimuisha jinsia na/au makundi yaliyotengwa kihistoria, kama vile watu wa kiasili.

Lakini, ufadhili wa kuwezesha mipango na mikakati hii kutimia bado haiutiliwi maanani. Usambasaji wa kimataifa wa fedha za kukabiliana na hali katika nchi zinazoendelea ni mara 5 hadi 10 chini ya makadirio yanayohitajika na pengo linaendelea kupanuka. Usambasaji wa fedha za kukabiliana na hali katika nchi zinazoendelea ulifikia Dola za Marekani bilioni 29 katika mwaka wa 2020, kama ilivyoripotiwa na nchi wafadhili, ongezeko la asilimia 4 ikilinganishwa na mwaka wa 2019. 

Usambasaji wa fedha za kukabiliana na hali katika mwaka wa 2020 ulipungua kwa angalau Dola za Marekani bilioni 17 ukipungua na dola bilioni 100 zilizoahidiwa kutolewa kwa nchi zinazoendelea.  Uharakishaji mkubwa unahitajika ikiwa kuongezeka maradufu kwa usambasaji wa fedha wa mwaka wa 2019 kufikia mwaka wa 2025 kutafikiwa, kama ilivyohimizwa na Mkataba wa Hali ya Hewa wa Glasgow. 

Makadirio ya mahitaji ya kila mwaka ya kukabiliana na hali ni dola za Marekani kati ya bilioni 160 na bilioni 340 kufikia mwaka wa 2030 na dola za Marekani kati ya bilioni 315 na bilioni 565 kufikia mwaka wa 2050. 

Utekelezaji wa hatua za kukabiliana na hali – zimejikita katika kilimo, maji, mifumo ya ekolojia na sekta anuai – unaimarika lakini hauendani na mabadiliko ya tabianchi. Hata hivyo, bila kuimarisha ufadhili, hatua za kukabiliana na hali zinaweza kuzidiwa na madhara yanayoongeza ya mabadiliko ya tabianchi.

Mfumo unganishi

Ripoti hii inaonyesha kwamba kuzingatia uhusiano kati ya juhudi za kudhibiti na kukabiliana na athari – kuanzia kwa kuweka mikakati, ufadhili, na utekelezaji kunaweza kuongeza manufaa ya kushirikiana. Pia kudhibiti uwezekano wa hatari, kama vile kupitia nishati ya maji kupunguza utoshelezaji wa chakula au unyunyuziaji maji mimea kuongeza matumizi ya nishati.

Kujitolea kikamilifu kisiasa kunahitajika ili kuimarisha uwekezaji na matokeo yake. Majanga kama vile vita nchini Ukrainia na COVID-19 haviwezi kuruhusiwa kupunguza juhudu za kimataifa za kuimarisha udhibiti. Utashi wa kisiasa ambao haujawahi kushuhudiwa na uwekezaji wa muda mrefu zaidi wa kukabiliana na hali unahitajika kwa haraka ili kukomesha kupanuka kwa pengo la kukabiliana na hali hiyo. 

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)

UNEP ni mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira kote duniani. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano wa utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.

Kwa taarifa zaidi tafadhali waliliana na:

Keisha Rukikaire, Mkuu wa Habari na Vyombo vya Habari, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa