Pixabay
02 Dec 2020 Toleo la habari Nishati

Ni sharti serikali ulimwenguni zipunguze uzalishaji wa nishati ya visikuku kwa asilimia 6 kwa mwaka ili kupunguza hali hatari ya ongezeko la…

Nairobi/Seattle, December 2, 2020 - Makala maalum ya Production Gap Report – kutoka kwa mashirika makuu ya utafiti na Umoja wa Mataifa – inaonyesha kuwa kujiimarisha baada ya COVID-19 ni fursa mzuri kwa nchi kubadili mienendo ili kudhibiti viwango vya joto wakati wa uzalishaji wa makaa ya mawe, mafuta na gesi na kuvidhibiti visizidi nyuzijoto 1.5.

Nchi zinapanga kuongeza uzalishaji wa nishati ya visukuku kwenye muongo ujao, hata kama utafiti unaonyesha kuwa ulimwengu unahitaji kupunguza uzalishaji wake kwa asilimia 6 kwa mwaka ili kudhibiti ongezeko la joto duniani lilizidi nyuzijoto 1.5, kwa mjibu wa ripoti ya mwaka wa 2020 ya 'Production Gap'

Ripoti hii iliyozinduliwa mara ya kwanza katika mwaka wa 2019, inapima pengo kati ya malengo ya Mkataba wa Paris na uzalishaji unaonuiwa kutekelezwa na nchi wa makaa ya mawe, mafuta na gesi. Inaonyesha kuwa pengo la “production gap” linasalia kuwa kubwa: nchi zinapanga kuongeza uzalishaji wa nishati ya visukuku zaidi ya maradufu katika mwaka wa 2030 zaidi inavyohitajika ili kudhibiti joto duniani lilizidi nyuzijoto1.5.

Makala ya kipekee yaliyotolewa mwaka huu yanaangazia athari za jangaa la COVID-19 – na mipango na mikakati ya serikali ya kujiimarisha na kuboresha uchumi– kuhusiana na uzalishaji wa makaa ya mawe, mafuta na gesi. Inatolewa wakati mwafaka ambao mabadiliko yanahitajika, kwa sababu janga hili linahitaji hatua za dharura kutoka kwa serikali – na wakati ambapo chumi kuu ikijumuisha China, Japan na Korea Kusini, zimetoa ahadi za kutozalisha gesi chafuzi kabisa. 

"Mioto ya ajabu kutokea kwenye misitu, mafuriko, kiangazi na majanga mengine mabaya kutokana na hali ya hewa, ni ukumbusho tosha wa kwa nini tunahitaji kufaulu kukabiliana na majanga kwa mazingira. Tunapojiandaa kuimarisha chumi baada ya jangaa la korona, kuwekeza kwenye nishati inayozalisha kiwango kidogo cha gesi ya ukaa na kwenye miundo msingi ina manufaa kwa chumi, kwa afya na kwa hewa safi," alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP). "Ni sharti serikali zichukue fursa hii kwa kuhakikisha chumi na mifumo yake ya nishati inaacha kutumia nishati ya visukuku, na kujiimarisha vyema ili kuwa na mustakabali endelevu, wenye haki na ulio dhabiti.

Ripoti hii ilitolewa na Taasisi ya Mazingira ya Stockholm (SEI), Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo Endelevu (IISD), Taasisi ya Maendeleo Nje ya Nchi, E3G, na UNEP. Watafiti mbalimbali walishiriki kwenye uchanganuzi na uhariri, na walitoka katika vyuo mbalimbali na mashirika mengine ya utafiti.

"Utafiti huu unaonyesha wazi kuwa tutakumbwa na athari mbaya kwa mazingira iwapo nchi zitaendelea kuzalisha nishati ya visukuku kwa viwango vilivyopo, bila kuzingatia mipango yao ya kuongeza," alisema Michael Lazarus, mwandishi mkuu wa ripoti hii na Mkurugenzi wa Kituo cha Marekani cha SEI. "Utafiti unatoa masuhuhisho kwa njia ya wazi: sera za serikali zinazopunguza mahitaji na usambasaji wa nishati ya visukuku na kusaidia jamii zinazovitegemea. Ripoti hii inatoa hatua ambazo serikali zinawezachukua kwa sasa ili kuwa na mabadiliko ya haki na yenye usawa bila kutumia nishati ya visukuku."

Matokeo makuu ya utafiti huu yanajumuisha:

  • Ili kuhakikishajoto linasalia kuwa na nyuzijoto 1.5, dunia itahitaji kupunguza uzalishaji wa nishati ya visukuku kwa takribani asilimia 6 kwa mwaka kati ya mwaka wa 2020 na mwaka wa 2030. Hata hivyo, nchi zinapanga na kunuia kuongeza viwango angalau kwa asilimia 2 kwa mwaka, hali ambayo kufikia mwaka wa 2030 itakuwa zaidi ya maradufu ua viwango inavyopaswa ili kutoziti nyuzijoto 1.5.
  • Kati ya mwaka wa 2020 na mwaka wa 2030,  uzalishaji wa makaa ya mawe, mafuta na gesi duniani ni sharti upungue kwa asilimia 11, asilimia 4, na asilimia 3, mtawalia ili kufanya joto kutozidi nyuzijoto 1.5.
  • Janga la COVID-19 – na masharti ya “kutotoka nje” ili kupunguza maambukizi – vipepeleka kupungua kwa uzalishaji wa nishati ya visukuku kwa mda katika mwaka wa 2020. Lakini mipango ya kabla ya korona na hatua za kujiimarisha baada ya korona ni ishara ya pengo linaloongezeka la uzalishaji wa nishati ya visukuku duniani, na kuhatarisha mazingira vibaya.
  • Kufikia sasa, serikali za G20 zimeahidi zaidi ya dola za Marekani bilioni 230 kutumiwa kukabiliana na korona kwa sekta zinazoshughulika na uzalishaji na matumizi ya nishati ya visukuku duniani, pesa zaidi kuliko zile zinazotolewa kwa wanaotumia nishati isiyochafua mazingira (takribani dola za Marekani bilioni 150). Waundasera ni sharti wakabiliane na mwenendo huu ili kufikia malengo ya mazingira.

"Hali ngumu iliyosababishwa na ongezeko la bei ya mafuta mwaka huu pia inaonyesha kuwa maeneo na jamii zinazotegemea nishati ya visukuku ziko hatarini. Njia pekee ya kuepukana na mtego huu ni kuwa na uchumi anuai usiotegemea tu nishati ya visukuku. Ajabu ni kuwa katika mwaka wa 2020 tulishuhudia serikali nyingi zikiongeza maradufu nishati ya visukuku na kuongeza hatari zilizopo," alisema Ivetta Gerasimchuk, mwandishi mkuu wa ripoti anayesimamia usambasaji wa nishati endelevu kwenye IISD. "Badala yake, serikali zinapaswa kuelekeza fedha za kujiimarisha baada ya korona kuwezesha kuwa na chumi zanazotegemea vitu mbalimbali na kuanza kutumia nishati isiyochafua mazingira iliyo na manufaa ya kipindi kirefu kwa chumi na kwa ajira. Hii inaweza kuwa changamoto kuu katika karne ya 21, lakini ni muhimu na inaweza kutekelezeka.”

Ripoti hiyo pia inaonyesha jinsi ambavyo ulimwengu unaweza kuacha kutumia nishati ya visukuku kwa njia iliyo na usawa, huku juhudi kubwa zikitarajiwa kutoka nchi tajiri zilizo na taasisi zenye uwezo wa kufanya hivyo na hazitegemei mno uzalishaji wa nishati ya visukuku. Baadhi ya wazalishaji wakubwa wa nishati ya visukuku kwenye kundi hili, ikijumuisha nchi za Australia, Canada na Marekani, ni baadhi ya nchi zinazotaka kuongeza usambasaji wa nishati ya visukuku.

Nchi ambazo zinategemea mno nishati ya visukuku na hazina uwezo wa kujimudu zitahitaji msaada wa kimataifa ili kuleta mabadiliko kwa njia iliyo na usawa, ripoti hiyo pia inaonyesha njia zinazoweza kutumika.

"Kupunguza uzalishaji wa nishati ya visukuku kwa kiwango kinachoenda sambamba na malengo ya Paris kunahitaji msaada na ushirikiano wa kimataifa," alisema Cleo Verkuijl, Mtafiti anayefadhiliwa na SEI, ambaye pia ni mwandishi mkuu wa ripoti hii. "Nchi zinapotoa ahadi za kipekee za kushughulikia mazingira kwa Umoja wa Mataifa (UN) Kabla ya Kongamano la UN la Mabadiliko ya Tabianchi litakotokea mjini Glasgow katika mwaka wa 2021, zina fursa ya kujumuisha malengo na mikakati ya kupunguza uzalishaji wa nishati ya visukuku kwenye mipango hii, au kwenye NDCs."

Ripoti hiyo inaanisha maeneo sita yanayopaswa kushughulikiwa, na kutoa fursa kwa watungasera kupunguza matumizi ya nishati ya visukuku wanapoweka mikakati ya kujiimarisha baada ya janga la korona. Mbali na mambo mengine, zinaweza kupunguza msaada unaotolewa na serikali kwa nishati ya visukuku, kuweka vikwazo kwa uzalishaji wake, na kuhakikisha ufadhili unatolewa kwa uwekezaji kwenye nishati isiyochafua mazingira (huku wakiruhusu matumizi makubwa ya kaboni na masharti ya kufikia malengo ya kudumu ya mazingira).

"Ripoti hii inaonyesha hatua zinazoweza kuchukuliwa na serikali, ambazo zikitekelezwa pakubwa, zinaweza kusaidia kupunguza matumizi ya nishati ya visukuku. Inatoa mapendekez na masuluhisho yatakayowezesha kuzalisha bila kutegemea makaa ya mawe, mafuta na gesi," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa SEI Måns Nilsson. "Ni wakati wa kutafaka na kuweka mikakati ili kuwa na mustakabali bora."

MAKALA KWA WAHARIRI

Maoni Kuhusu Ripoti ya Production Gap

"Ripoti hii inaonyesha bila pingamizi lolote kuwa uzalishaji na matumizi ya makaa ya mawe, mafuta na gesi ni sharti yapungue kwa kasi iwapo tunataka kufikia malengo ya Mkataba wa Paris kuhuiana na mabadiliko ya tabianchi. Hii ni muhimu ili kuhakikisha kuwa katika siku zijazo kuna mazingira salama na dhabiti, na chumi endelevu katika nchi zote – ikijumuisha waathiriwa wakuu wakati wa kuhama kutoka matumizi ya nishati chafuzi na kuanza kutumia nishati isiyochafua mazingira. Ni sharti serikali zifanye kazi kuhakikisha kuwa zina chumi zinazotegemea vitu mbalimbali na kuwasaidia wafanyakazi, ikijumuisha kupitia mikakati ya kujuimarisha baada ya korona ambayo haitaruhusu matumizi ya nishati ya visukuku yasiyo endelevu na badala yake kushiriki manufaa ya chumi endelevu zisizochafua mazingira. Tunaweza na ni sharti tujiimarishe vyema kwa kushirikiana." – Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres

"Janga la korona limetikiza masoko ya nishati ni iwapo tutachukua fursa hii, tunaweza kuleta mabadiliko kwa kukusudia. Ijapokuwa baadhi ya nchi ziko mstari mbele kuondoa ruzuku inayotolewa kwa nishati ya visukuku na kudhibiti utafiti na uchimbaji wake, ni sharti kuwe na juhudi zaidi iwapo tunataka kupunguza pengo kati ya mipango iliopo ya uzalishaji wa nishati ya visukuku na ahadi za kushughulikia mazingira zilitolewa chini ya Mkata wa Paris wa Mazingira.  Kwa kufanya kazi kwa ushirikiano, serikali, kampuni na wawekezaji wanaweza kusimamia viwanda vya nishati ya visukuku kwa njia inayopunguza madhara na kuhakikisha kuwa mabadiliko yanafanyika kwa njia ya haki kwa wafanyakazi na jamii." – Mary Robinson, Rais Mstaafu wa Ireland and na Mwenyekiti wa Wazee

"Sayansi inaonyesha wazi kuwa uzalishaji wa nishati ya visukuku ni sharti upunguzwe mno ili kufikia malengo ya mazingira. Hali hii inapaswa kutokea kwa njia inayosimamiwa vizuri, ya haki, na usawa kote duniani. Serikali zinapaswa kuanzisha majadiliano na wafanyakazi na vyama vyao, na jamii zilizoathiriwa ili kutekeleza mikakati ya uhamiaji ya haki inayopunguza madhara makuu na kupata manufaa mengi iwezekenavyo ya matumizi ya nishati isiyochafua mazingira." – Ayuba Wabba, Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Muungano wa Wafanyakazi

Kuhusu Ripoti ya Production Gap 

Ripoti iliyoandikwa kwa kutumia kielelezo cha matoleo ya Ripoti ya Emissions Gap — na kuchukuliwa kama uchanganuzi kamilisho — ripoti hii inaonyesha mwanya mkubwa uliopo kati ya mipango ya nchi ya uzalishaji wa nishati ya visukuku na viwango vya kimataifa vya uzalishaji vinavyohitajika ili kudhibiti ongezeko la joto lisizidi nyuzijoto 1.5.

Kuhusu Taasisi ya Mazingira ya Stockholm
Taasisi ya Mazingira ya Stockholm ni taasisi ya kimataifa ya utafiti inayojishughulisha na sera ya kimataifa kuhusiana na masuala ya mazingira na maendeleo katika ngazi ya eneo, ya kitaifa na ya kanda ambayo imekuwepo kwa zaidi ya robo ya karne. SEI huunga mkono maamuzi ya kuleta maendeleo endelevu kwa kutumia sayansi na sera.

Kuhusu UNEP
Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) ni mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira.  Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.

Kuhusu Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo Endelevu  
Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo Endelevu (IISD) ni taasisi ya kujitegemea ambayo imewahi kushinda tuzo, inapigania masuluhisho kwa changamoto kuu za mazingira yanayotokana na utafiti. Dira yetu ni kuwa dunia isiyobagua ambapo watu na mazingira yatanawiri; dhima yetu ni kuharakisha mabadaliko duniani yatakasababisha matumizi ya maji safi, chumi bora na mazingira dhabiti. Na ofisi mijini Winnipeg, Geneva, Ottawa na Toronto, kazi yetu huathiri maisha ya watu kwenye angalau nchi 100. 

Kuhusu ODI
ODI ni taasisi  ya kimataifa inayojitegemea inayofanya kazi ili kuhakikisha kuwa kuna dunia endelevu iliyo na amani ambapo kila mtu atanawiri. Sisi hutegemea idhibati na mawazo yanayotokana na utafiti na wabia ili kukabiliana na changamoto, kutoa suluhu na kuleta mabadiliko

Kuhusu E3G
E3G ni taasisi ya kimataifa inayojitegemea ya kushughulikia mabadiliko ya tabianchi Ulaya. Sisi ni waundamikakati wakuu kuhisiana na siasa na uchumi unaotegemea siasa kuhusiana na mabadiliko ya taianchi, tunaojitolea kuhakikisha kuwa kuna mazingira salama kwa wote. Tunafanya kazi inayohusiana na hali ya hewa ili kukabiliana na changamoto na kuleta suluhu ili kuwa na mazingira salama. Lengo letu ni kuhakikisha siasa kuhusiana na mazingira, chumi, na sera zinachukuliwa.

Kwa Taarifa zaidi tafadhali wasiliana na:

Emily Yehle,Afisa Mkuu wa Mawasiliano, Taasisi ya Mazingira ya Stockholm
News and Media unit, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)