Pixabay
24 Nov 2020 Toleo la habari Nishati

Sekta ya Mafuta na Gesi yajitolea kuweka mikakati mipya ya kufuatilia, kuripoti na kupunguza uzalishaji wa methani

Nairobi/Brussels/New York, Novemba 23 - Kupitia hatua zitakazosaidia kukabaliana na chanzo kikubwa cha changamoto za mazingira zinazoweza kutatuliwa, wahusika wakuu katika sekta ya mafuta na gesi walikubaliana leo kuripoti kuhusu uzalishaji wa methani kupitia njia mpya ya uwazi na ya kiwango cha juu.

“Ili kufaulu kutokuwepo na uzalishaji wa gesi chafu kabisa, tunahitaji juhudi za kila mmoja wetu. Sekta ya Mafuta na Gesi inastahili kuchukua hatua dhabiti. UNEP imejitolea kuimarisha juhudi za kupunguza uzalishaji wa gesi ya methani, na tunapongeza viongozi wa kampuni ambazo zimejiunga na mfumo wetu wa kuripoti,"  alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP. "Tunatarajia kuona hatua zitakazowesha ahadi za kupunguza uzalishaji wa gesi hii.”

Methani ikienda angani, ina uwezo wa kuunda gesi ya ukaa, ikiwa na uwezo mara 80 zaidi wa kuongeza kiwngo cha joto ikilinganishwa na kaboniksidi kwa kipindi cha miaka 20. Hatua za kupunguza uzalishaji wa methani inaweza kusabababisha upunguzaji wa kiwango cha joto, na kusaidia kupunguza gesi ya ukaa kwenye sekta ya nishati na sekta ya uchukuzi huku kiwango cha hewa kikiboreshwa.

Kadri Simson, Kamishna wa Muungano wa Ulaya (EU) alisema "Ninafuraha mno kushuhudia sekta ya nishati ikichukua hatua za dharura kuhusiana na uzalishaji wa methani. Kujitolea wazi kupima na kufuatilia uzalishaji wa gesi chafu ni hatua muhimu ya kwanza ya kupunguza kiwango chake kikubwa na ninajivunia kuona hatua ambazo tumepiga kwa ushirikiano. Kutia sahihi kulikotokea siku ya leo ni matokeo ya kwanza chini ya mikakati ya methani ya Kamisheni hiyo. Kuna hatua nyingi zaidi za kuchukuliwa ili kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwenye mfumo mzima wa biashara na nina matumaini ya kushirikiana kufanya kazi na wabia kutoka Ulaya na wabia wa kimataifa ili kufikia lengo hili."

Ubia wa Methani Kutoka kwa Mafuta na Gesi (OGMP) ni mradi wa Muungano wa Mazingira na Hewa Safi (CCAC) unaoendeshwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Kamisheni ya Ulaya (EC), na Mfuko wa Kushughulikia Mazingira (EDF). Tayari Kampuni 62 zinazopatikana kwenye mabara tano na zinazokadiria asilimia 30 ya uzalishaji wa mafuta na gesi duniani zimejiunga na ubia huo. Mfumo mpya wa OGMP2.0 ni mfumo wa viwango vipya vya kimataifa vya kutumia kuripoti ambao utaboresha kuripoti na kutoa taarifa kwa njia ya wazi kuhusu uzalishaji wa methani katika sekta ya mafuta na gesi.

"Pongezi kwa kampuni 62 zilizojitolea kupima, kuripoti na kupunguza uchafuzi zinapoendelea na shughuli zake na hata kushirikiana na kampuni zingine. Viwango hivi vitatumiwa kama msingi Ulaya na kwengineko ili kuhakikisha sekta ya mafuta inachukua hatua zinazoweza kutekelezeka kwa dharura kwa mazingira yetu," alisema Fred Krupp, Rais wa Mfuko wa Kushughulikia Mazingira.

Ubia wa Methani Kutoka kwa Mafuta na Gesi 2.0

Msingi wa juhudi hizi ni mfumo mpana wa kuripoti kuhusu methani utakaorahisishia watu wa ngazi za juu, wawekezaji na umma kufuatilia na kulinganisha vizuri utendakazi kwenye kampuni mbalimbali kupitia njia ambazo hazingewezekana hapo awali.

“Kupunguza uzalishaji wa methani ni hatua muhimu ya kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa. Kama kigezo kinachoweza kuzalisha matunda haraka, OGMP 2.0 ina manufaa mengi kwa makampuni katika sekta yetu yaliyo tayari kuimarisha upunguzaji wa uzalishajiwa gesi chafu katika mfumo mzima wa biashara. Tunatarajia kuendelea kufanya kazi na wabia wote waohusika, kwa maana ni kupitia tu kwa ushirikiano na mashirika ya kimataifa, mashirika ya uraia na serikali tutafaulu kufikia malengo yetu," alisema Claudio Descalzi, Afisa Mkuu Mtendaji wa ENI.

Jinsi inapotikana katila mikakati ya methani ya EU, Kamisheni ya Ulaya inalenga kufafanua zaidi mapendekezo ya kisheria kuhusu upimaji, kuripoti na udhibitishaji wa lazima kwa uzalishaji wowote wa gesi chafu ya methani, kwa kuzingatia mfumo wa OGMP 2.0.

Cha muhimu, OGMP 2.0 haijihusishi na utendakazi wa kampuni husika, lakini pia biashara zinginezo anuai zinazomilikiwa kwa pamoja zinazochangia uzalishaji mkubwa. Mfumo wa OGMP 2.0 unajishughulisha na sekta mzima ya mafuta na gesi, sio tu uzalishaji wake, pia usafirishaji wake, uandaaji wake na hata usafishaji – sekta zilizo na uwezekano mkubwa wa kuzalisha gesi chafu ambayo mara nyingi hupuuzwa wakati wa kuripoti.

Lengo lake ni kuwezesha sekta ya mafuta na gesi kupunguza uzalishaji wa methani katika kipindi cha muongo mmoja ujao katika njia ya uwazi kwa mashirika ya uraia na serikali.

“Kupunguza uzalishaji wa methani ni muhimu ili kuleta mabadiliko ya matumizi ya nishati. Ubia huu mpya umewezesha kushiriki matendo mazuri, hasa kuhusiana na mali ya kampuni isiyotumika, na kuimarisha ufuatiliaji,” alisema Patrick Pouyanné, Mwenyekiti na Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Total. “Hii ni hatua mpya ya kukabiana na uzalishaji wa methani na sekta yetu imejitolea mno kufaulisha mradi huu.”

Ili kufikia malengo ya kimataifa ya mazingira, OGMP 2.0 inalenga kupunguza uzalishaji wa methani katika sekta hiyo kwa asilimia 45 kufikia mwaka wa 2025, na kati ya asilimia 60 na 75 kufikia mwaka wa 2030.

Masuhisho yasiyokuwa ghali

Kwa mjibu wa Shirika la Kimataifa la Nishati (IEA), takribani robo tatu za uzalishaji wa methani zinaweza kupunguzwa kwa kutumia teknolojia zilizopo, takribani nusu yake ikifanyika bila kutumia gharama yoyote. Kupunguza uzalishaji wa methani katika sekta ya nishati kwa asilimia 90 kunaweza kusaidia kupunguza ongezeko linalokisiwa kuongezeka kwa ushuru mbili kufikia mwaka wa 2050.

Kupunguza uzalishaji wa methani kwa asilimia 75 kunaweza kusaidia kupunguza uzalishaji wa kabonkisidi kwa gigatani 6 kila mwaka - takribani asilimia kumi ya uzalishaji wa gesi ya ukaa katika mwaka wa 2019, ikijumuisha mabadiliko katika matumizi ya ardhi.

Mwangalizi Mpya wa kazi

UNEP na Kamisheni ya Ulaya wanakamilisha mipango ya kuanzisha mfumo wa kujitegemea wa Uchunguzi wa Kimataifa wa Uzalishaji wa Methani (IMEO). IMEO itakusanya na kuchanganua data mbalimbali kuhusiana na uzalishaji wa methani, ikijumuisha data inayotolewa na kampuni wanachama wa OGMP, ili kuimarisha upunguzaji wa gesi ya methani inayozalishwa kote duniani. Kwa kusaidia viwanda na serikali kote duniani kukabiliana na changamoto zinazohusiana na uzalishaji ulioripotiwa, taasisi hiyo ya uchunguzi itaboresha utapikanaji wa data ya kuaminika kuhusu uzalishaji wa methani na kuimarisha hatua za kukabiliana na hali hii.

MAKALA KWA WAHARIRI

Nukuu Zaidi

“Sisi kama Wintershall Dea tunafuraha isiyokuwa na kifani kutia sahihi OGMP 2.0. Ni muhimu kuwa na data ya kuaminika inayopatikana kwa njia ya wazi kuhusu uzalishaji wa methani. OGMP 2.0 inatupa fursa ya kushiriki na wabia wetu wa kimataifa kuhusu vyanzo vya uzalishaji wa methani – kwa kutumia msingi dhabiti. Tunaunga mkono Kamisheni kwa kulenga kuzindua kampeni kampeni itaakayowezesha watu zaidi kujiunga nasi. Yunatarajia kujadiliana nao na kufaulisha mpango huu.” alisema Mehren, Afisa Mkuu Mtendaji wa Wintershall.

“Uwekezaji wa kipindi cha miaka 30 umewezesha kupungunguza uzalishaji wa methani kabisa. Kwa kushauriana na OGMP kupitia kwa Thüga Energienetze, schwaben netz and Energienetze Bayern tunaunga mkono malengo ya mradi huu muhimu na tunataka kushiriki matendo mazuri kutoka kwa Thügagroup. Tunaamini kuwa kupitia utekelezaji wa hatua kuu za kupunguza uzalishaji wa gesi chafu bali matumizi ya nishati jadidifu na kupunguza gesi ya ukaa kwenye mfumo wetu wa kupitisha waya za umeme, itakuwa hatua muhimu ya kufikia Malengo ya Paris,” alisema Michael Riechel, Afisa Mkuu Mtendaji wa Thüga Aktiengesellschaft.

“GRTgaz inalenga kupunguza uzalishaji wetu wa methani kwa theluthi moja kwa kuzingatia viwango vya mwaka wa 2016. Karibu tunafaulu na tunajivunia kwa hatua tulizopiga. Pia, tunafahamu kuwa safari bado ni ndefu na tunanuia kuweza kugawa na 5 viwango kati ya mwaka wa 2016 na 2025. Wafanyakazi wa GRTgaz na wenzao, ambao ni wanachama wa OGMP 2.0 wanafahamu wanachohitaji kufanyia sayari na wako tayari kufanya hivyo,” alisema Thierry Trouvé, Afisa Mkuu Mtendaji wa GRTgaz

Kupata kauli zaidi, tafadhali tembelea: http://ogmpartnership.com/sites/default/files/files/Companies_Statements.pdf

Kuhusu OGMP

OGMP, lilizinduliwa na Baraza Kuu la Mazingira la Umoja wa Mataifa katika mwaka wa 2014, ilibuniwa na Muungano wa Mazingira na Hewa Safi (CCAC) kama mradi wa hiari ili kusaidia kampuni kupunguza uzalishaji wa methani katika sekta ya mafuta na gesi. Ikisimamiwa na UNEP, OGMP ni mbia wa pekee aliye na wadau mbalimbali wanaofanya kazi kuripoti kuhusu uzalishaji wa methani na kutoa utaratibu wa kusaidia makampuni kushughulikia uzalishaji wa methani kutokana na shughuli za mafuta na gesi kwa kutumia mbinu zinazoaminika za kisayansi ili kusaidia kampuni wanachama kuonyesha wadau zilivyoweza kupunguza.

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

UNEP in mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyoKwa maelezo zaidi: www.unep.org

Kuhusu Kamisheni ya Ulaya 

Kamisheni ya Ulaya (EU) ni tawi linalojitegemea la Muungano wa Ulaya, linalojishughulisha na kuunda mapendekezo ya utengenezaji wa sheria Ulaya na kufuatilia utekelezaji wake. Mbali na kusimamia sera ya EU na ketengea EU fedha, Kamisheni hiyo hupigania maslahi ya Muungano wa Ulaya kwa kuiwakilisha katika ngazi ya kimataifa. 'Green Deal' ya Ulaya ni nguzo ya Kamisheni ya Ulaya ya kuwezesha Ulaya kuwa bara la kwanza kujali mazingira kikamilifu. Kwa hivyo, malengo ya mazingira na malengo ya nishati ni muhimu wakati wa kuunda sera za Kamisheni. Kwa taarifa zaidi: https://europa.eu/

Kuhusu Mfuko wa Kushughulikia Mazingira

Mojawapo ya mashirika makuu ya kimataifa yasikuwa ya biashara, Mfuko wa Kushughulikia Mazingira hutoa masuluhisho yanayoleta mabadiliko kwa changamoto kuu za mazingira. Kufaulu, EDF huleta pamoja wabia kutoka sekta za sayansi, uchumi, sheria wabunifu kutoka kwa sekta binafsi. Ikiwa na zaidi ya wanachama milioni 2.5 kwenye ofisi zinazopatikana Marekani, China, Mexico, Indonesia na Muungano wa Ulaya, wanasayansi, wataalamu wa masuala ya uchumi, mawakili na wataalamu wa sera wa EDF wanafanya kazi kwenye nchi 28 ili kufanyia kazi masuluhisho tunayotoa. Ungana nasi kwenye Twitter @EnvDefenseFund

Kuhusu Muungano wa Mazingira na Hewa Safi

CCAC  ni muungano wa pekee wa wabia unaoshirikisha serikali, mashirika ya kimataifa, kampuni za biashara, taasisi za kisayansi na mashirika ya uraia yanayojitolea kuimarisha ubora wa hewa na kutunza mazingira kwa kupunguza vichafuzi vya mazingira vinavyofanya kazi kwa mda mfupi - methani, kaboni nyeusi, haidroflorokaboni na ozoni ya tropoferiki. Huendesha miradi 11 katika sekta kuu zinazozalisha gesi chafu na kutumika kama chombo  cha kuwezesha kuunda kushiriki na kutekeleza masuhuhisho yanayopunguza ongezeko la joto haraka, kuimarisha maisha ya watu, kuhakikisha kuwa kuna maendeleo endelevu kwa vizazi vijavyo. Kwa taarifa zaidi: https://ccacoalition.org/en

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na: 

Keishamaza Rukikaire, Msimamizi wa Habari na Vyombo vya Habari, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), rukikaire@un.org

Tiy Chung, Afisa wa Mawasiliano, Sekretarieti ya Muungano wa Mazingira na Hewa Safi Tiy.Chung@un.org

Laura Catalano, Naibu wa Rais, Mawasiliano katika Mfuko wa Kushughulikia Mazingira, lcatalano@edf.org

Ewelina Hartstein, Naibu wa Mkuu wa Kitengo cha ENER A.2, Mawasiliano ya Sera na Mahusiano kati ya Taasisi, Ewelina.HARTSTEIN@ec.europa.eu

Terry Collins, Mshauri wa Media, +1-416-878-8712, tc@tca.tc