Credit: Pexels / Belle Co
15 Dec 2020 Toleo la habari Malengo ya Maendeleo Endelevu

UNEP yatangaza wanamazingira saba wa kipekee kama washindi wa tuzo lake la Vijana Bingwa Duniani

Credit: Pexels / Belle Co
  • Tuzo la Vijana Bingwa Duniani hutolewa kila mwaka kwa wajasiriamali saba walio na umri usiozidi miaka 30 walio na maono dhabiti ya kusababisha mabadiliko ya kudumu kwa mazingira.
  • Washindi saba, kutoka katika maeneo mbalimbali kote ulimwenguni, hupokea hisa zisizo na riba ya kudumu, ushauri na msaada wa mawasiliano ili kuimarisha juhudi zao.

Nairobi, Disemba 15, 2020 – Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) leo lilitangaza vijana saba ambao ni wanasayansi, wahandisi, wajasiriamali na wanaharakati kutoka pembe zote za dunia kama washindi wa mwaka wa 2020 wa tuzo la Vijana Bingwa Duniani.

Wakitoa masuluhisho ya jinsi ya kupata maji kutoka kwa hewa, kuunda vibamba kutoka kwa plastiki, na kushawishi wavuvi kuondoa matani ya plastiki kutoka baharini, watu hawa wanaosababisha mabadiliko wanaonyesha jinsi ambavyo maono ya uvumbuzi yakijumuisha juhudi za kipekee yanavyoweza kukabiliana na baadhi ya changamoto kuu zinazokumba mazingira.

"Kote duniani, vijana wako mstari mbele kutoa wito wa kutoa suluhu ya kipekee kwa dharura kwa aina tatu ya changamoto zinazokumba dunia; mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai na uchafuzi  –tunapaswa kuwasikiliza," alisema Inger Andersen, Katibu mtendaji wa UNEP. "Tunapoingia katika muongo tunaopaswa kuchukua hatua za kupunguza uzalishaji wa gesi chafu na kutunza na kuboresha mifumo ya ekolojia, Washindi wa Tuzo la Vijana Bingwa Duniani ni ishara tosha kuwa sisi sote tunaweza kutoa mchango wetu kwa kuanzia tuliko na kwa kutumia kile tulicho nacho. Juhudi zozote tunazochukua kwa naiaba ya mazingira ni muhimu, na kila mtu kote duniani anapaswa kuwajibika na kutumia fursa iliopo.  

Washindi saba, wote wakiwa na umri usiozidi miaka 30, walichaguliwa na wataalamu ambao ni waamuzi wa kimataifa baada ya kupendekezwa na umma. Washindi wa mwaka wa 2020 wa Tuzo la Vijana Bingwa Duniani ni:

  • Afrika: Nzambi Matee (Mkenya mwenye umri wa miaka 29), mhandisi wa vifaa na msimamizi wa kampuni ya Gjenge Makers, inayounda vifaa endelevu vya kujengea kwa bei nafuu kutoka kwa plastiki iliyotumika na mchanga.
  • a and the Pacific: Xiaoyuan Ren (China, 29) leads MyH2O, a data platform that tests and records the quality of groundwater across a thousand villages in rural China into an app so residents know where to find clean water. The platform also educates communities about sources of contamination and connects villages with potable water companies.Asi
  • Asia na Pasifiki: Vidyut Mohan (Mhindi mwenye umri wa miaka 29) alishirikiana na wenzake kuanzisha Takachar, kampuni inayotengeneza mitambo  inayoweza kuhamishwa ya kuboresha bayomasi, hali inayowezesha wakulima kujipatia pesa zaidi na kuzuia uchomaji wa taka katika maeneo wazi kwa kuunda nishati, mbolea kaboni hai kutoka taka ya mimea.
  • Ulaya: Lefteris Arapakis (Mgiriki mwenye umri wa miaka 26) alianzisha kampuni ta Enaleia, ambayo kikosi chake hutoa mafunzo, kujengea uwezo na kutuza wavuvi kutoka kwa jamii ya wenyeji ili wakusanye taka kutoka baharini, hali inayopelekea ongezeko la idadi ya samaki na uboreshaji wa mifumo ya ekolojia. Kampuni ya Enaleia hutumika kama kielelezo za kutengenezea bidhaa za mtindo wa kisasa kama vile soksi na mavazi ya kuogelea kutoka kwa plastiki.
  • Amerika ya Latini na Karebian: Max Hidalgo Quinto (kutoka Peru, mwenye umri wa miaka 30) alianzisha Yawa, kampuni inayotengeneza mitambo ya upepo inayoweza kuhamishwa inayowezesha kupata maji lita 300 kutoka kwa unyevunyevu na ukungu.
  • Amerika Kaskazini   Niria Alicia Garcia (Mmarekani  mwenye umri wa miaka 28), hushirikiana na wanaharakati kutoka katika jamii za kiasili kuratibu- shughuli ya Run 4 Salmon akitumia mtandao ili kuelimisha watu kuhusu historia ya samoni wa chinook katika mji wa Sacramento unaopatikana katika jimbo la California eneo lililio na maji mengi, na kuhamasisha watu kuhusu mfumo huu muhimu wa ekolojia, spishi zake na watu wanaonufaika.
  • Asia Magharibi: Fatemah Alzelzela (kutoka Kuwait, mwenye umri wa miaka 24) alianzisha Eco Star, mradi wa shirika lisilokuwa la biashara ambalo huchukua taka na kutoa miti kwa majumba, shule na mashirika ya biashara nchini Kuwait. Tangu kuzinduliwa kwake mwaka wa 2019, shirika la Eco Star limetumia taka ya vyuma, ya makaratasi na ya plastiki tani 130 kuundia bidhaa.

Tangazo la washindi wa Tuzo la Vijana Bingwa Duniani limetokea baada ya kutangazwa kulikotokea siku ya ijumaa kwa washindi sita wa tuzo la Mabingwa wa Dunia, tuzo la ngazi ya juu  linalotolewa na Umoja wa Mataifa kwa heshima ya mazingira. Viongozi wa kipekee ambao juhudi zao zimesababisha mabadiliko chanya kwa mazingira hutuzwa.

Kwa kuhamasisha kuhusu kazi muhimu inayofanywa na wanaharakati wa mazingira, Tuzo la Vijana Bingwa Duniani- sehemu ya kampeni ya UNEP ya #ForNature (#TutunzeMazingira) linalenga kutoa motisha kwa watu zaidi na kuchombea vijana zaidi kuchukua hatua za kushughulikia mazingira tunapoelekea  Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Oboreshaji wa Mifumo ya Ekolojia (2021-2030), Kongamano la Umoja wa Mataifa la Bayoanuai (COP 15) lilitakalofanyika mjini Kunming mwezi wa Mei mwaka wa 2021, na Kongamano la Umoja wa Mataifa la Mabadiliko ya Tabianchi (COP26) mjini Glasgow katika mwezi wa Novemba mwaka wa 2021.   

 

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)

UNEP ni mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira duniani. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.

Kuhusu Vijana Bingwa Duniani

Tuzo la Vijana Bingwa Duniani ni mradi mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa wa kushirikisha vijana kwenye utatuaji wa changamoto kuu zinazokumba mazingira. Washindi saba walitangazwa katika mwezi wa Disemba mwaka wa 2020. Washindi hupokea msaada wa kifedha na ushauri ili kufanikisha miradi yao inayohusiana na mazingira. Tangu kuanzishwa kwake katika mwaka wa 2017, wanamazingira wa kipekee 28 kutoka pembe zote za dunia wametuzwa.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:

Keishamaza Rukikaire, Msimamizi wa Habari na Vyombo vya Habari, UNEP