Pixabay
16 Dec 2020 Toleo la habari Matumizi bora ya rasilimali

Uzalishaji wa gesi chafu kutoka katika sekta ya ujenzi uliongezeka mno, ila kujiimarisha baada ya korona bila kuchafua mazingira kunaweza…

  • CO2 emissions increased to 9.95 GtCO2 in 2019. The sector accounts for 38% of all energy-related CO2 emissions when adding building construction industry emissions
  • Direct building CO2 emissions need to halve by 2030 to get on track for net zero carbon building stock by 2050
  • Governments must prioritize low-carbon buildings in pandemic stimulus packages and updated climate pledges
  • Uzalishaji wa CO2 uliongezeka na kufikia GtCO2 9.95 katika mwaka wa 2019. Sekta hiyo inakadiria asilimia 38 ya jumla ya uzalishaji wa CO2  inahusiana na nishati tukijumuisha uzalishaji kutokana na sekta ya ujenji
  • Uzalishaji wa CO2 wa moja kwa moja unahitaji kupungua maradufu ili kutozalisha gesi ya ukaa kufikia mwaka wa 2050
  • Serikali sharti zitilie kipaumbele majengo yasiyozalisha ukaa mno wakati zinapotenga fedha za kujiimarisha baada ya janga la korona na zinapotoa ahadi za kushughulikia mazingira.

Nairobi, Disemba 16, 2020 – Uzalishaji wa gesi chafu kutoka katika sekta ya ujenzi uliongezeka mno katika mwaka wa 2019, na kupunguza uwezo wa sekta hiyo kupunguza kasi ya mabadiliko ya tabia nchi na uwezo wa kufikia malengo ya Mkataba wa Paris kikamilifu, kwa mjibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo.

Hata hivyo, fedha zinazotengwa ili kutumiwa kujiimarisha baada ya korona ni fursa kwa ubunifu katika sekta ya ujenzi na kuweka viwango vya kushughulikia majengo mapya, na hivyo kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa kasi. Ahadi zinazotarajiwa kupokelewa kwa kuzingatia Mkataba wa Paris- zinazojulikana kama Ahadi Zilizowekwa na Taifa au NDCs- pia ni fursa ya kuimarisha hatua zilizopo na kuongeza ahadi mpya sekta ya ujenzi na majengo.

Ripoti ya The 2020 Global Status Report for Buildings and Constructionkutoka kwa Muungano wa Kimataifa wa Ujenzi na Majengo (GlobalABC), inaonyesha kuwa ijapokuwa matumizi ya nishati katika sekta ya ujenzi duniani yalisalia kuwa dhabiti mwaka baada ya mwaka, uzalishaji wa kabonikisidi (CO2 ) kutokana na matumizi ya nishati yaliongezeka na kufikia GtCO2  9.95 katika mwaka wa 2019. Hii ilitokana na kuepuka kutumia makaa ya mawe, mafuta, bayomasi ya kiasili na kuanza kutumia umeme, vitu ambavyo vilikuwa na kiwango kikubwa cha gesi ya ukaa kutokana na kuhitaji nishati nyingi wakati wa uzalishaji.

Kwa kuongezea uzalishaji kutoka kwa sekta ya ujenzi kwa uzalishaji unaotokana na utendakazi, sekta hiyo inakadiriwa kuchangia asilimia 38 ya jumla ya uzalishaji wa CO2  duniani kutokana na matumizi ya nishati.

"Ongezeko la uzalishaji wa gesi chafu katika sekta ya ujenzi na majengo inaonyesha kuwa kuna umuhimu wa kuimarisha mikakati kwa dharura mara tatu zaidi ili kupunguza mahitaji ya nishati wakati wa ujenzi, kutozalisha gesi ya ukaa katika sekta ya nguvu za umeme na kuweka mikakati ya itakayopunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa kutokana na jinsi vitu vinavyozalishwa,” alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP).

"Kutenga fedha za kujiimarisha baada ya korona kunaweza kutuwezesha kupiga hatua tunazohitaji kwa kasi, aliongezea. "Kuwezesha sekta ya ujenzi na majengo kuzalisha kiwango kidogo cha gesi ya ukaa kutapunguza kasi ya mabadiliko ya tabianchi na kuwezesha uchumi kunufaika kwa kuimarfika, na kwa hivyo serikali zote zinapaswa kutilia suala hili maanani."

Kuwezesha kutozalisha gesi ya ukaa kufikia mwaka wa 2050, Shirika la Kimataifa la Nishati (IEA) linakadiria kuwa uzalishaji wa moja kwa moja wa CO2  unahitaji kupungua maradufu ili kutozalisha gesi ya ukaa kufikia mwaka wa 2030 ili kupungua kwa asilimia 50 na uzalishaji usiotokea moja kwa moja katika sekta ya ujenzi upungue kwa asilimia 60. Hii inamaanisha kuwa uzalishaji wa CO2 katika sekta ya ujenzi unahitaji kupungua kwa asilimia 6 kila mwaka hadi mwaka wa 2030, na ulifikia takribani asilimia 7 kwenye sekta ya nishati duniani katika mwaka wa 2020 kutokana na janga la korona.

Cha kusikitisha, kifaa kipya cha GlobalABC cha kufuatilia hali ya hewa kwenye majengo – kinachozingatia mikakati kama vile matumizi mwafaka ya nishati wakati wa uwekezaji kwenye majengo na kiwango cha matumizi ya nishati jadidifu kwenye majengo – kinaonyesha kuwa kiwango cha uimarishaji katika kila mwaka kinadidimia. Kilipungua maradufu kati ya mwaka wa 2016 na mwaka wa 2019. Kuwezesha sekta ya ujenzi kutozalisha gesi ya ukaa kufikia mwaka wa 2050, wahusika wote katika sekta nzima ya ujenzi wanapaswa kuimarisha hatua za kutozalisha gesi ya ukaa na athari zake mara tano zaidi.

Ijapokuwa juhudi za matumizi mwafaka ya nishati hazijaweza kukabiliana na ongezeko kwenye sekta hii, kuna ishara chanya na fursa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, matokeo ya ripoti hiyo yaonyesha.

Uwezo wa kuimarisha uchimi bila kuchafua mazingira

Ripoti ya hivi majuzi ya Emissions Gap Report 2020 kutoka kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) inaonyesha kuwa kuimarisha uchumi bila kuchafua mazingira kunaweza kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa kwa asilimia 25 kutoka kwa ile inayotabiriwa kufikia mwaka wa 2030 na kuifanya dunia kuwa karibu kufikia lengo la nyuzijoto 2 kama ilivyo kwenye Mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya tabianchi.  Hatua zaidi zinahitajika ili kufikia nyuzijoto 1.5.

Serikali zinaweza kusaidia kukabiliana na hali hii kwa kuweka mikakati ya kutozalisha gesi ya ukaa wakati wa ujenzi kama sehemu ya kujimairisha baada ya janga la korona  –  kuongeza ada ya kukarabati majengo, kutoa nafasi za kazi, na kuongeza thamani ya mali isiyohamishika.

Ijakuwa shughuli za ujenzi zilipungua kwa asimia kati ya 20 na 30 katika mwaka wa 2020 ikilinganishwa na mwaka wa 2019 kutokana na janga la korona, takribani asilimia kumi ya nafasi za kazi kwa jumla zimepotezwa au ziko hatarini kwenye sekta ya ujenzi, programu za kuwajibisha sekta ya ujenzi na majengo zinaweza kubuni nafasi za kazi, kuarisha uchumi, na kuimarisha biashara. Chini ya mikakati yake ya Kujuimarisha kwa Njia Endelevu, IEA inakadiria kuwa nafasi 30 za kazi zinaweza kubuniwa kwa sekta za uzalishaji wa bidhaa na ujenzi kwa kila dola milioni moja zinazowekezwa kwenye uboreshaji au kwenye mikakati kabambe wakati wa ujenzi.

Ahadi mpya za NDC ni fursa kwa juhudi kuchukuliwa haraka

Nchi nyingi bado hajijatoa ahadi mpya wa NDCs. Ujenzi unasalia kuwa sekta kuu isiyokuwa na sera dhahiri za kukabiliana na gesi ya ukaa licha ya umuhimu wake kwa uzalishaji wa CO2  duniani. Kwa nchi ambazo zimetoa NDC, nchi 136 zimetaja majengo, nchi 53 zimetaja nishati mwafaka, nchi 38 pekee zimetaja jinsi ya kutumia nishati wakati wa ujenzi.

Serikali za taifa ni sharti zionyeshe kujitolea kwake kupitia NDCs, kuweka mikakati ya kudumu kuhusiana na tabianchi na kuweka sheria zitakazowezesha kutozalisha gesi ya ukaa katika sekta ya ujenzi. Hii inamaanisha kutoa kipaumbele kwa kanuni za ujenzi zinazozingatia utendakazi anbazo ni sharti zitekelezwe na hata kutoa vibali vya uidhinishaji na kufanya kazi kwa karibu na serikali za mtaa ili kuharakisha matumizi na utekelezaji wake.

Ongezeko la uwekezaji kwenye nishati mwafaka

Katika mwaka wa 2019, gharama ya ujenzi wa majengo kwa kutumia nishati mwafaka iliongezeka kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka mitatu, na matumizi mwafaka ya nishati katika sekta ya ujenzi kote ulimwenguni yakiimarika na kufikia dola za marekani bilioni USD 152 katika mwaka wa 2019, asilimia 3 zaidi ikilinganishwa na mwaka uliotangulia.

Hiki ni kiwango kidogo tu cha dola za Marekani trilioni 5.8 zilizotumika katika sekta ya ujenzi na majengo, ila kuna ishara chanya kwenye sekta nzima ya uwekezaji kuwa kutozalisha gesi ya ukaa kwenye majengo na kutumia nishati mwafaka kama sehemu ya mikakati ya uwekezaji.

Kwa mfano kati ya kampuni 1,005 za mali isiyohamishika, wajengaji, REITS, na fedha zinazowakilisha mali zaidi ya doala za Marekani trilioni 4.1 zinazosimamiwa na kuripotiwa kwa "The Global ESG Benchmark for Real Assets katika mwaka wa 2019, asilimia 90 ilizingatia viwango vya majengo yasiyochafua mazingira kwenye ujenzi na shughuli za ujenzi.

Majengo yasiyochafua mazingira yanaashiria fursa za kimataifa katika sekta za ujenzi kwenye muongo ujao, inayokadiriwa na IFC kuwa dola za Marekani trilioni 24.7 kufikia mwaka wa 2030.

Mapendekezo zaidi

Mbali na kupendekeza kujiimarisha baada ya korona bila kuchafua mazingira na kutoa NDCs mpya, ripoti hiyo pia inapendekeza kuwa wamiliki wa majumba na washirika ya biashara yanapaswa kutumia mbinu za kisayansi wakati wa kufanya maamuzi na kushirikiana na wadau wakati wa kutoa ramani za ujenzi, wakati wa ujenzi, wakati wa utendakazi na utumiaji ili kushirikiana na kujengeana uwezo.

Wawekezaji wanapaswa kuchunguza upya uwekezaji kwenye mali isiyohamishika kwa kutumia nishati kwa njia mwafaka na kupunguza gesi ya ukaa.

Wahuka wengine katika mfumo mzima wa ujenzi wanapaswa kutumia bidhaa zinazoweza kutumiwa tena na tena ili kupunguza hitaji la vifaa vya ujenzi na kupunguza gesi ya ukaa na kutumia masuluhisho yanayojali mazingira ili kuwa na majengo dhabiti.

Nukuu Zaidi

“Sekta ya ujenzi ni muhimu katika kukabiliana na changamoto zinazoikimba dunia kama vile mabadiliko ya tabianchi, changamoto zinazokumba uchumi kutokana na janga la COVID 19, kuboresha maisha ya watu na udhabiti wa miji yetu. Kwa Mexico, utekelezaji wa hatua za kuimarisha hali ya joto na ya matumizi ya nishati katika sekta ya ujenzi ni muhimu ili kuwa na maendeleo endelevu.” alisema Sergio Israel Mendoza, Meneja Mkuu wa Sekritarieti ya Mexico ya Mazingira na Malighafi inayoshughulika na Ukuzaji wa Mazingira, Miji na Utalii (SEMARNAT)

“Ni sharti tushughulikie swala la uzalishaji wa gesi ya ukaa katika sekta ya ujenzi na majengo kwa dharura, unaokisiwa kuwa asilimia 40 ya jumla ya uzalishaji wa gesi chafu duniani. Ni sharti tuelezee serikali kuhusu hali hii kwenye mkutano wa COP26 ili kuwezesha kubuniwa kwa sera na kufanya maamuzi yatakayowezesha kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa katika sekta hii”, alisema Nigel Topping, Mhamasishaji kutoka Uingereza wa hali ya hewa ya kiwango cha juu. “Tunahitaji kukabiliana na vyuma na saruji. Kuamua iwapo vyuma na saruji, vitu vinavyosababisha gesi ya ukaa vitaendelea kutumika katika siku zijazo itatagemea kasi ya ubunifu wa teknolojia mpya isiyosumbua katika sekta hiyo. Kuna ahadi kabambe zilizotolewa chini ya Mradi Unaotokakana na sayansi zilizotolewa na kampuni kuu zinazotengeneza vitu vya kutumiwa inayoweza kuzingatiwa kushawishi sekta hiyo kuchukua hatua zaidi.”

 

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu Muungano wa Kimataifa wa Ujenzi na Majengo (GlobalABC)

(GlobalABC) ni jukwaa kuu la kimataifa linaloweza kutumiwa na serikali, sekta binafsi, mashirika ya uraia na kwa mashirika ya kimataifa ili kuimarisha juhudi zitakazowezesha kutozalisha gesi ya ukaa, kuwa na majengo mwafaka na dhabiti kwenye sekta ya ujenzi. Muungano wa Kimataifa wa Ujenzi na Majengo (GlobalABC) ulibuniwa baada ya Mkutano wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa wa mwaka wa 2015.

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

UNEP ni mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira duniani. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo. 

For further information please contact:

Keishamaza Rukikaire, Msimamizi wa Habari na Vyombo vya Habari, UNEP, +254 722 677747,

Terry Collins, Mshauri wa Media, +1-416-878-8712, tc@tca.tc