UNEP
27 Feb 2024 Toleo la habari Youth, education & environment

Wanaohitajika: Vijana wanaokabiliana na changamoto za aina tatu duniani,

Upendekezaji  wa tuzo la mwaka wa 2024 la UNEP la VijanaBingwa wa Dunia umefunguliwa

  • Tuzo la Vijana Bingwa wa Dunia hutolewa kwa heshima ya watu binafsi kati ya umri wa miaka 18 na miaka 30 wanaoonyesha uwezo wa kipekee wa kusaidia kutunza mazingira.
  • UNEP inatafuta vijana saba wanaotekeleza mawazo na masuluhisho ya kipekee yanayoonyesha uwezo wa mazingira kushughulikia changamoto za aina tatu duniani za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai na uharibifu wa mazingira, na uchafuzi.
  • Vijana Bingwa wa Dunia watatambulishwa kwa umma, kupokea mtaji wa kuanzia, mafunzo, ushauri na ufikiaji wa waleta mabadiliko duniani.  
  • Upendekezaji unaanza tarehe 27 Februari hadi tarehe 5 Aprili mwaka wa 2024.  

Nairobi, Februari 27, 2024 – Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) leo limezindua wito wa kupendekeza watakaowania tuzo lake la Vijana Bingwa wa Dunia linalotambua mchango wa vijana na uwezo wao wa kipekee wa kuongoza juhudi za kutunza mazingira.

Mwaka huu, UNEP inatafuta vijana saba -kati ya umri wa miaka 18 na miaka 30- wanaoonyesha kujitolea kutunza mazingira na wanaosimamia miradi inayotunza na kuboresha mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuboresha mifumo ya ekolojia, na kukabiliana na chafuzi. Awamu ta mwaka huu ya matuzo ya Vijana Bingwa wa Dunia inaendeshwa kwa ushirikiano wa Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia, wakiungwa mkono na Mfumo mpya Wa Kimataifa wa Bayoanuai.

Vijana Bingwa watakaochaguliwa na UNEP watapokea dola za Marekani 20,000 kama mtaji wa kuanzia, fursa ya kuhudhuria mikutano ya ngazi ya juu ya Umoja wa Mataifa, uwezo wa kufikia jamii ya wataalam wa kimataifa, na mafunzo ya kina na ushauri maalum wa kufanikisha mawazo yao makubwa ya kushughulikia mazingira. UNEP inatafuta wajasiriamali vijana, wanasayansi, wataalamu wa masuala ya uchumi, wasanii, na wazungumzaji kutoka katika matabaka mbalimbali maishani ambao wana mawazo makubwa, ya kijasiri - kwa manufaa ya mazingira, binadamu, na kwa mustakabali usio na uchafuzi. Ili kuonyesha kujitolea na uwezekano wa mradi kutekelezeka, wanaowania watarajiwa lazima wawe wamefanyia kazi mawazo yao kikamilifu kwa angalau miezi sita.

"Wajasiriamali, wasomi, wabunifu, na wanaharakati vijana wa kipekee wanahitaji kuungwa mkono ili kuwezesha sayari kuimarika," Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP alisema. "UNEP inatafuta mawazo ya ubunifu zaidi katika kizazi hiki, kutoka kwa nyanja zote na kila eneo ulimwenguni, ambayo yanarekebisha uhusiano wetu na mazingira."

Washindi wa awali wa tuzo la UNEP la Vijana Bingwa wa Dunia ni pamoja na Adjany Costa, ambaye alitengeneza kielelezo cha kuigwa na jamii katika mojawapo ya vitovu vya mwisho vya wanyamapori mashariki mwa Angola, Lefteris Arapakis, kutoka Ugiriki, anayefunza, kuwajengea uwezo na kuwatia motisha wavuvi wakongwe na wapya katika Mediterania kukusanya plastiki kutoka baharini, na Eritai Kateibwi, ambaye Mradi wake wa Te Maeu unalenga kutengeneza mfumo wa kilimo wa hydroponiki ulio na athari chache ili kuwa na mazao mabichi Kiribati.

Watoto na vijana wanastahimili athari mbaya zaidi za changamoto za aina tatu duniani za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai na uchafuzi, pamoja na ongezeko la ukosefu wa usawa na ukosefu wa ajira. Iwapo vijana watakuwa na sayari inayoweza kuwezesha maisha katika siku zijazo, watahitaji ufikiaji bora wa ufadhili, ushirikiano na ubia, na ushawishi mkubwa kwa uundaji wa sera za mazingira. 

Mpango wa Vijana Bingwa wa Dunia unafadhiliwa na Elephant17.org, mpango unaolenga ‘Paying It Forward For Climate ulioanzishwa na Chris Kemper. Bw. Kemper ni Mtetezi wa Ubia wa UNEP na Mwenyekiti, Mwanzilishi na Afisa Mkuu Mtendaji wa Palmetto Clean Technology, ambaye, kupitia mpango huu, analenga kuchangia kuwajengea uwezo vijana wanaoendelezza utunzaji wa mazingira kote duniani.  

"Ili kufikia malengo ya Mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi, sehemu kubwa ya ulimwengu ni lazima ianze kutumia teknolojia mpya na masuluhisho ya kiasili, na mabadiliko kama haya ya kimfumo yanahitaji ujasiriamali na nishati ambayo wajasiriamali wanaoibuka wanabuni," Alisema Chris Kemper. "Ninaamini kuwa wajasiriamali ni chanzo cha msukumo, nguvu na kujitolea kunakohitajika kufanya mabadiliko yanayohitajika na chanya katika ulimwengu wa leo. Nina shauku ya kuona matokeo ambayo Mabingwa wapya watazalisha."

Kutuma maombi ya kuwania tuzo la UNEP la Vijana Bingwa wa Dunia kunaanza tarehe 27 Februari hadi tarehe 5 Aprili, 23:59 masaa ya Afrika Mashariki (EAT) kupitia tovuti ya Vijana Bingwa wa Dunia.

 

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu  Tuzo la UNEP la Vijana Bingwa wa Dunia
Tuzo la UNEP la Vijana Bingwa wa Dunia ni tuzo lililoundwa ili kuhuisha matarajio ya wanamazingira vijana. Tuzo hili hutolewa kila mwaka kwa vijana saba wanaojitolea kutoka kote ulimwenguni wenye mawazo ya kipekee ya kutunza na kuboresha mazingira. (ongeza kipeperushi)

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)
UNEP in mhamasishaji mkuu wa masuala ya mazingira. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.

Kuhusu Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia

Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia 2021-2030 unatoa wito wa kutunzwa na kuboreshwa kwa mifumo ya ekolojia kote ulimwenguni, kwa manufaa ya watu na mazingira. Muongo unaosimamiwa na UNEP kwa ushirikiano na FAO, unalenga kukomesha uharibifu wa mifumo ya ekolojia, na kuiboresha ili kufikia malengo ya kimataifa. Utaisha mwaka wa 2030, makataa ya SDGs na wakati wa mwisho  unaorejelewa na wanasayansi kama fursa ya mwisho ya kuzuia madhara mabaya zaidi ya mabadiliko ya tabianchi.

 

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na: 

Kitengo cha Habari na Vyombo vya Habari, UNEP