25 Oct 2019 Tukio Misitu

Jinsi ya kutunza wanyamapori huku jamii jirani zikinufaika—Mradi wa kwanza wa REDD+ duniani

Eneo la Tsavo linajulikana kutokana na ukame wa mda mrefu. Maisha ni magumu kwa binadamu na mifugo.

Siku moja, mfanyabiashara kutoka Marekani aliyezuru Kenya alipendezwa mno na wanyamapori wake lakini akagundua jinsi jamii zinazoishi karibu zinavyoteseka. Alianzisha 'Wildlife Works' na katika mwaka wa 2011 mradi wao wa 'Kasigau Corridor Project' ukawa wa kwanza wa Kupunguza Uchafuzi Unaoatokana na Ukataji wa Miti na Uharibifu wa Misitu (REDD+). Ni mradi wa kwanza ulimwenguni kuidhinishwa na mashirika mawili yanayokadiria ubora wa bidhaa—shirika la the Verified Carbon Standard na la the Climate Community and Biodiversity Alliance. Kwa ushirikiano, mashirika haya mawili hutathmini kila kipengele cha mradi, ikiwa ni pamoja ya jinsi yakupima kupungua kwa uzalishaji wa hewa ya ukaa, na pia kuchunguza iwapo iwapo jamii pia inanufaika bila ubaguzi wala upendeleo. Shirika la Wildlife Works lilibuni methodolojia ya mradi  wa Kasigau Corridor Project ili kulinganisha gesi ya ukaa katika maeneo kame yaliyo na misitu na misitu iliyo kwenye maeneo ambayo hushuhudia mvua.

"Haikuwa kazi rahisi," asema Cara Braund, Meneja wa Hifadhi ya  Wildlife Works. "Lakini tulifahamu tunachohitaji kufanya ili mradi wa REDD+ ufaulu. Tulikuwa na changamoto ya kupata ardhi ya kutumia kutoka kwa wamiliki wa ardhi (kukodisha mashamba), tulipokea vitisho hadharani (kutoka kwa watu wanapenda kukata miti au kufyeka misitu ili wafanye ukulima, na pia kutoka kwa watu wanaoharibu misitu kupata mbao na kuchoma makaa. Pia tulikuwa na uhusiano mwema na jamii ambao tulinuia kudumisha. Kwa hivyo tunashirikana na jamii hizi ili kutoa njia mbadala za mapato.”

A local of Taita Taveta County in Kenya works as a fashion manufacturer in Wildlife works Conservation company business. The conservation company established the project design development and a framework for income generating activities. The project provides various alternative livelihood trainings such as soap production, fashion manufacturing, basket making, and climate smart agriculture
Mwanakijiji kutoka Kaunti ya Taita Taveta nchini Kenya hutengeneza mitindo mbalimbali ya mavazi katika kampuni ya Wildlife Works Conservation. Kampuni hiyo ilianzisha mradi wa mitindo ya mavazi na kusaidia watu kuwa na mapato. Mradi huo hutoa mafunzo mbalimbali ya kusaidia watu kuwa na mapato kama vile utengenezaji wa sabuni, utengenezaji wa mitindo mbalimbali za mavazi, utengenezaji wa vikapu, na kufanya kilimo cha kisasa kinachojali mazingira. Picha na Mradi wa UN-REDD.

Njia mbadala ya kuishi ili kubadili meinendo

Kampuni ya Wildlife Works iliweka kanuni za jinsi ya kuendesha mradi na utaratibu utakaofuatwa ili kuzalisha mapato. Walielewana kwa hiari kushirikisha wamiliki wa mashamba na wanakijiji kwa mradi—jumla ya watu wapatao laki moja wananufaika kutokana na mradi huu. Hakuna anayepaswa kuathirika kwa njia ghasi kutokana na mradi na kuna mfumo uliowekwa wa kutatua mizozo.

Ni sharti wamiliki wa mashamba watunze miti na hawaruhusiwi kuruhusu ukataji wa miti, kulisha mifugo kupindukia na wala uchomaji wa makaa katika eneo la mradi.

Mradi huo hutoa mafunzo mbalimbali ya kusaidia watu kuwa na mapato kama vile utengenezaji wa sabuni, utengenezaji wa mavazi, utengenezaji wa vikapu, kilimo cha kisasa kinachojali mazingira (jinsi ya kupandikiza miti, jinsi ya kupanda miche, unyunyiziaji wa maji, kilimo wima na kutumia dawa ya kuangamiza dudu isiyodhuru mazingira kama vile mshubiri, pilipili, mwarobaini au matawi ya tumbaku), jinsi ya kuanzisha hifadhi za kuwavutia watalii, na kadhalika. Una waajiriwa wapatao 350, wakijumuisha takribani askaripori 100 wanaotunza misitu na wanyamapori. Baadhi yao wamewahi kuwa wawindaji haramu na wachomaji wa makaa waliobadili mienendo yao.

Grazing elephants  in Tsavo West National park, Kenya.
Ndovu wakila majani katika hifadhi ya  Kitaifa ya Tsavo Magharibi. Picha na Mradi wa UN-REDD.

Chanzo kikuu ya kukuwezesha kupata pointi za gesi ya ukaa

Mradi wa Kasigau Corridor REDD+ kwa sasa unazalisha idadi iliyodhibitishwa ya gesi ya ukaa 1,800,000, inayojulipana pia kama pointi au tani, kwa mwaka. Ndiyo kubwa kwa miradi miwili ya REDD+ nchini Kenya. Wao huuza pointi zao kwa hiari ambapo watu binafsi au mashirika kama vile BNP Paribas na Shirika la Fedha Duniani hununua ili kupunguza gesi ya ukaa. Ifikiapo mwaka wa 2020, itakuwa soko iliyoidhinishwa, hali itakayowezesha kuimarisha mauzo.

Ili kugawana fedha zinazotokana na mauzo ya pointi, theluthi moja huwaendea wamiliki wa mashamba. Wildlife Works inagharamia fedha za kuendesha mradi na faida inagawanywa katikati kati ya jamii husika na wawekezaji. Jamii, kupitia kwa wanakamati wa jamii huamua jinsi ya kutumia fedha wanazopata kutokana na mauzo ya pointi: kupokea mafunzo, kwa miradi ya kuboresha afya au kwa elimu (majengo ya shule au kufadhili wanafunzi). Kila kamati ina angalau wanawake wawili na vijana wawili ili kujumuisha kila mtu.

"Miradi ya  REDD+ iliyofaulu kama vile mradi wa Kasigau Corridor ni muhimu na inaonyesha kuwa utunzaji wa misitu na wanyamapori una manufaa makubwa kwa jamii. Kupanda miti zaidi na kushughulikia mazingira mashambani ni muhimu iwapo tunataka kufaulu kukabiliana na changamoto za mazingira na kutunza bayoanuai," anasema Tim Christophersen, msimamizi wa  tawi la Maji Safi Ardhi na Tabianchi la Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa . 

Mradi huu umenufaika kutokana na kuongezeka kwa elimu inayohusu mradi wa REDD+ na kutokana na kukubalika kwake sana nchini Kenya. Mpango wa Kitaifa wa UN-REDD ulisaidia kuanzisha mradi huu utakaodumu kwa miaka 30. Kwa kuwa umekuwepo kwa miaka karibu 10 bado umesalia na miaka zaidi ya ishirini. Mradi huu unalenga kuwa endelevu kwa wamiliki wa mashamba na kwa jamii ili kuwawezesha kuwa na njia mbadala ya mapato na kupokea maarifa ya kujikimu na wasiwe na sababu ya kutumia misitu kupata fedha kupitia njia zinazoenda kinyume cha sheria kama vile ukataji wa miti ili kupata mbao, uchomaji wa makaa na uwindaji haramu.

Maudhui Yanayokaribiana