UNEP
31 May 2023 Video Kushughulikia kemikali na uchafuzi

Côte d'Ivoire ni mwenyeji wa Siku ya Mazingira Duniani Mwaka wa 2023

UNEP

 

Siku ya Mazingira Duniani Mwaka wa 2023 inandaliwa na Côte d'Ivoire kwa ushirikiano na Uholanzi.

Kaulimbiu itaangazia masuluhisho ya uchafuzi wa plastiki chini ya kampeni ya #KomeshaUchafuziWaPlastiki

Tarehe 5, Juni mwaka wa 2023 ni maadhimisho ya miaka 50 ya Siku ya Mazingira Duniani baada ya kuzinduliwa na Baraza la Umoja wa Mataifa katika mwaka wa 1972. Kwa kipindi cha miongo mitano iliopita, siku hii imekua na kuwa mojawapo ya majukwaa makubwa zaidi duniani yanayohamasisha kuhusu masuala ya mazingira. Mamilioni ya watu hushiriki kupitia mtandaoni na kupitia juhudi nyanjani.

Unaweza kushiriki vipi?

Kuanzia kwa shule na makundi ya jamii hadi kwa mashirika ya biashara, miji na serikali, kila mtu anahimizwa kuandaa na kusajili hafla au juhudi karibu na tarehe 5 Juni kwa ajili ya Siku ya Mazingira Duniani.

Tumia na kushiriki Mwongozo wa Vitendo wa Uchafuzi wa Plastiki. Unaonyesha hatua ambazo sisi sote tunaweza chukua kusitisha na kukabiliana na madhara yanayosababishwa na uchafuzi wa plastiki.

Unaweza pia kueneza ujumbe na kuwatia wengine moyo kwa mitandao ya kijamii