Mandhari

Kuhusu maji

Maji hufunika zaidi ya thuluthi mbili za sayari, ila maji yanayopatikana kwa urahisi – kutoka mitoni, maziwani, kwenye ardhioevu na chemichemi za maji – ni chini ya asilimia 1 ya maji yanayopatikana kote duniani.

Kadiri idadi ya watu duniani inavyoongezeka, ndivyo mahitaji ya maji yanavyoongezeka – kutumiwa kunywa na usafi wa mazingira, kwa kilimo na uzalishaji wa nishati na kwa matumizi mengineyo. Wakati uo huo, shughuli za binadamu na mabadiliko ya tabianchi yanavuruga mizunguko asilia ya maji, na kutoa shinikizo kwa vyanzo vya maji safi ambavyo ni mifumo yetu ya ekolojia ya maji safi. Uchafuzi, ukuzaji wa miundomsingi na uchimbaji wa malighafi huzidisha changamoto zilizopo.

Soma zaidi

Kazi yetu

Malengo ya Maendeleo Endelevu Yanayokaribiana

Watu na wabia

Kazi ya UNEP katika sekta ya maji safi hujumuisha mambo mengi na huunganisha kazi ya shirika zima, kuanzia kwa makao yake makuu mjini Nairobi hadi kwa ofisi zake za kikanda na vituo vya ushirikiano kote duniani. Ikiongozwa na Vipaumbele vya Kimkakati vya Maji Safi, kazi yetu inategemea uelewa wa kimsingi kwamba vyanzo vya maji huathiri kwa njia mbalimbali, na ni muhimu katika kukabiliana na changamoto za aina tatu duniani za uchafuzi, uharibifu wa bayoanuai na mabadiliko ya tabianchi.

Tunashirikiana na wabia kadhaa kama vile Kituo cha Ushirikiano cha UNEP-DHI kuhusu Maji na Mazingira, ili kusaidia Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa. Huwa tunashirikiana na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa, ikijumuisha UN-Water, shirika linaloratibu kazi ya Umoja wa Mataifa kuhusu maji na usafi wa mazingira. Washirika wetu kutoka nje ni pamoja na mashirika ya biashara, taasisi za kutoa mafunzo na mashirika yasiyo ya kiserikali.