Unsplash/freepik
27 Jul 2021 Tukio Kushughulikia kemikali na uchafuzi

Jinsi kuunda mbolea kunavyoweza kutusaidia kupunguza athari zetu kwa mazingira

Unsplash/freepik

Kila mwaka, kote ulimwenguni, tani bilioni 1.3 za chakula hupotea au kuharibika, kwa mjibu wa Kigezo cha Kupima Uharibifu wa Chakula cha Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP). Kigezo cha Kupimia Uharibifu wa Chakula

Baa la njaa linapoongezeka kutokana na janga la COVID-19, kuna haja ya kupunguza uharibifu wa chakula kwa dharura.

Ripoti iliyochapishwa mwezi wa Julai mwaka wa 2021 na Shirika la Chakula na KilimoMpango wa Chakula Duniani, Shirika la Afya Duniani na mashirika mengine ya UN inaonyesha kuwa thuluthi moja ya idadi ya watu ulimwenguni - watu wengi wapatao milioni 811 - walikuwa na utapiamlo katika mwaka wa 2020, ikiwa ni ongezeko la watu milioni 118 milioni ikilinganishwa na mwaka wa 2019.

Mbali na kuzidisha baa la njaa na ukosefu wa chakula, kupotea na kuharibika kwa chakula huchangia changamoto tatu zinazoikumba dunia na kuhatarisha hatima yetu kwa jumla - mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai, na uchafuzi wa mazingira.

Ijapokuwa upoteaji na uharibifu hutokea katika mfumo mzima wa chakula, watu binafsi na familia wana kile wanachoweza kufanya. Kwa kuzingatia ukweli kuwa upoteaji na uharibifu wa tani milioni 570 hutokea majumbani, juhudi zao ni muhimu.

Miongozo iliyotolewa na UNEP na Taasisi ya Mikakati ya Mazingira Duniani (IGES) inaonyesha kuunda mbolea ni mojawapo ya njia bora zaidi ya kushughulikia taka inayoweza kuoza huku ikipunguza athari kwa mazingira.

Kutumia njia mwafaka kuunda mbolea kutoka kwa taka inayoweza kuoza tunayozalisha katika maisha yetu ya kila siku - chakula kisichokulika au kisichotumiwa - kunaweza kupunguza utegemezi wa mbolea za kemikali, kusaidia kurudisha rutuba mchangani, na kuboresha uhifadhi wa maji na usafirishaji wa virutubishi hadi kwenye mimea.

Kwa ujumla, kwa kupunguza uharibifu wa chakula, kuunda mbolea pia husaidia kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa inayoathiri mabadiliko ya tabianchi. Upoteaji na uharibifu wa chakula huzalisha takribani asilimia kati ya 8 na10 ya uzalishaji wa gesi ya ukaa duniani huku matumizi ya ardhi na rasilimali za maji kupindukia vikiweka shinikizo kwa bayoanuai

“Hatuingiliani vizuri na mazingira,” anaeleza Doreen Robinson, Mkuu wa Wanyamapori wa UNEP. “Wanadamu wanaendelea kunyakua na kusaza, ila mazingira huendelea tu kutoa.”

Badala yake, anasema, "tunahitaji kuunda bidhaa kutoka kwa bidhaa zingenezo na kudumisha uhai wake na kuwezesha vitu kuendelea kutumiwa."

 

Akitazamia mabadiliko ulimwenguni, Katibu Mkuu wa UN, António Guterres ataitisha Mkutano wa UN wa Mifumo ya Chakula katika mwezi wa Septemba  mwaka wa 2021. Kuwezesha kuleta mabadiliko kuelekea mifumo ya chakula yenye manufaa kwa lishe, kwa mazingira na maishani, Shirika la Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UNEP) huchangia Programu ya Mifumo Endelevu ya Chakula ya Mtandao wa Sayari Moja,  inayoongoza ukuzaji wa mwongozo fwa utengenezaji wa sera shirikishi na kuboresha kwa utawala; na mshirika wa Jukwaa la Ubia wa Kuleta Mabadiliko,  inayoelimisha wafadhili na watungasera na kukuza uvumbuzi. UNEP pia husimamia kipengee cha uharibifu wa chakula cha Lengo la Maendeleo Endelevu la 12.3, uwajibisha nchi wanachama kupunguza uharibifu wa chakula unaofanywa na kila mtu kwa nusu katika ngazi ya ununuzi na matumizi; na hivi sasa inaunda Kigezo cha Kigezo cha kupimia Uharibifu wa Chakula, kihifadhi data cha taarifa kuhusu uharibifu wa chakula ulimwenguni kinachowezesha nchi kufuatilia maendeleo ya kufikia Lengo.