REUTERS / Goran Tomasevic
17 Nov 2020 Tukio Kutumia mazingira kushughulikia tabianchi

Kushiriki faida kutoka kwa maziwa ya magadi nchini Kenya

REUTERS / Goran Tomasevic

Ziwa Bogoria linalopatikana kwenye eneo la Bonde la Ufa nchini Kenya, ni ziwa la magadi – lina chumvi na alikali nyingi, kwa hivyo samaki hawawezi kuishi ndani. Lina umuhimu mkubwa kwa masuala ya kiroho na kwa utamaduni wa  Waendorois, ambao wamekuwa wakilitunza kwa karne nyingi. Lakini katika miaka ya hivi majuzi waligundua kuwa ziwa hilo linaweza kuwa na manufaa makubwa.

Ziwa hilo – lililo maarufu kutokana na korongo na vijito vya maji safi – lina vijiumbe maradhi vya kipekee na vijiumbe vya kipekee vinavyoweza kutoa vimeng'enya vyenye thamani. Vimeng'enya vimeondolewa na kutumiwa na makampuni yanayopatikana Ulaya na Marekani kuunda viua vijasumu, sabuni na rangi ya nguo.  Baadhi ya kampuni hizi zimekumbwa na kesi kwa kutogawia Kenya fedha wanazozipata.

Mkataba wa Nagoya

Katika mwaka wa 2014, Kenya iliidhinisha Mkataba wa Nagoya, makubaliano ya kimataifa yanayotekeleza upatikanaji na kugawana mapato kutoka rasilimali viumbe kutokana na utafiti wa bayoteknolojia na maendeleo. Mkataba huo unaadhimisha miaka 10 mwaka huu.

People at a ceremony
Maadhimisho ya miaka 10 ya Mkataba wa Nagoya.- Waendorois. Picha: UNEP / Timothy Shitagwa

Kupitia msaada kutoka kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na Mfuko wa Mazingira Duniani, tangu mwaka wa 2014, Shirika la Huduma kwa Wanyamapori Nchini Kenya limekuwa likishirikiana na watafiti kutafuta vitu muhimu kutoka katika ziwa Magadi ili kuvitumia kuunda bidhaa kutoka kwa viumbe hai vya kutumika kutengeneza nguo na kemikali za kuua wadudu zinazotengenezwa kutoka kwa viumbe.

"Wanasayansi kutoka nchini Kenya wanatenga vimeng'enya vya kutumia kutengeneza nguo – kutengeneza nyuzi kutoka kwa pamba na hatimaye kutengeneza vitambaa vya nguo  – ili kuacha kutumia kemikali kama vile magadi zinazotumika kwa sasa. Matumizi ya dawa za kuua wadudu kutoka kwa viumbe wakati wa kufanya kilimo ni aina ya pili ya utafiti." anasema Levis Kavagi, mtaalamu wa bayoanuai wa UNEP ambaye ameshulikia mradi huu.

Chini ya Mkataba wa Nagoya, watafiti hao – kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi, Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta , na Chuo Kikuu cha Moi – walitakiwa “kupata kibali kwanza” kutoka kwa wenyeji kupitia mchakato wa mashauriano rasmi.

"Mkataba wa Nagoya uhakikisha kuwa kila mmoja anashirikishwa. Unatoa wito wa kushirikishwa kwa wenyeji na wadau, kwa kuzingatia mahitaji ya wanawake, watoto na watu wanaoishi na ulemavu," alisema Juliette Biao, Mkuu wa Ofisi ya UNEP ya Ukanda wa Afrika.

People at a ceremony
Maadhimisho ya miaka 10 ya Mkataba wa Nagoya.- Waendorois. Picha: UNEP / Timothy Shitagwa

Kufanya kazi kwa ushirikiano na jamii za wenyeji

UNEP imekuwa ikifanya kazi kwa ushirikiano na jamii ya Waendorois, wanaoishi karibu na Ziwa Bogoria, na wamekuwa wa msaada mno kwa mradi huu.

"Msaada kutoka kwa UNEP umewezesha jamii ya Waendorois kuandaa mkataba wake unaojumuisha vipengele vya bayolojia na vya utamaduni utakaotoa utaratibu utakaofuatwa na watafiti na matumiaji wengine wa rasilimali," alisema Eric Kimalit, mwenyekiti wa jamii ya Waendorois.

Kavaka Mukonyi, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Wanyamapori Nchini Kenya, ambaye ameshiriki kwenye mradi huu tangu ulipoanzishwa, alisema

"Safari ya Mkataba wa Nagoya haijakuwa rahisi. Ila matokeo yake yanafurahisha. Kupata kibali kutoka kwa wanajamii na kanuni zinazowekwa kwa pamoji chini ya mkataba huu vinatumiwa kama vielelezo na nchi nyinginezo barani Afrika katika mifumo yao ya kuhakikisha kupatikana na matumizi ya rasilimali inanufaisha pande zote."

Wabia kutoksa sekta binafsi

Mashirika ya sekta binafsiRIVATEX na Dudutech yamekuwa yakipima uwezo wa kufanya biashara ya vitu muhimu kutoka kwa viumbe hai vinavyopatikana kwenye ziwa kwa kuvitumia kutengeneza nguo na kemikali za kuua wadudu zinazotengenezwa kutoka kwa viumbe.

Kampuni ya Dudutech inafanya utafiti nyanjani na hivi karibuni itazindua mradi utakaowawezesha wakulima kufanya majaribio ya kemikali za kuua wadudu zinazotengenezwa kutoka kwa viumbe chini ya mradi huu. Majarabio hayo yanahitajika kabla ya kuidhinisha kemikali za kuua wadudu zinazotengenezwa kutoka kwa viumbe kuanza kuuzwa.

Chuo Kikuu cha Nairobi kimebainisha kuwa vimeng'enya vinavyeza kutumika kutengeneza ngozi na nguo kwa kutumia mbinu za kisasa maabarani.

Sasa inawezekana kutengeneza ngozi kutoka kwa wanyama viwandani kwa kutumia mbinu zisizodhuru mazingira na vimeng'enya vinavyofanya kazi kwa kasi, na kuepuka uchafuzi wa mazingira unaotokana na kemikali zinazotumika kutengeza vifaa vya ngozi," anasema Francis Mulaa kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi. "Tunafanya kazi kwa ushirikiano na Taasisi ya Utafiti Viwandani Nchini Kenya na kampuni ya RIVATEX kuimarisha vimeng'enya vya kutengeneza nguo.

Hifadhi ya Sampuli

Chini ya mradi huu, taifa ya Kenya limejenga kituo za kuhifadhi na kuanisha vimeng'enya katika Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta, kilicho na mitambo ya kisasa ya kiwango cha juu maabarani. Watafiti – wa ndani ya nchi na wale wa kimataifa – wanatarajiwa kutuma sampuli zao kwenye kituo hicho – kitakachosaidia kutafuta chanzo cha vitu vya kibayolojia  na kuwekea haki miliki na kulindwa isiigwe na watu wengine.

Kufaulu kwa mradi huu pia kumewavutua Magavana kutoka kwa Kaunti zingine mbili nchini Kenya – Kakamega na Laikipia – na zinanuia kuweka sera zinazofanana na mradi huu ili kunufaisha wenyeji wa maeneo hayo.

Mkataba wa Nagoya kuhusu Upatikanaji wa Rasilimali Zinazotokana na Viumbe na Ugawanaji wa Marupurupu Yanayopatikana kwa Njia Isiyobagua kutokana na Matumizi yake (ABS) na Mkataba wa Bayoanuai ya Kibayolojia ni makubaliano mbadala ya Mapatano kuhusu Bayoanuai.

Kwa taarifa zaidi kuhusu mradi wa Ukuzaji wa Bayoteknolojia ya Vijiumbe Maradhi kutoka kwa Maziwa ya Magadi nchini Kenya na kazi ya UNEP kuhusu Bayoanuai, tafadhali wasiliana na Levis Kavagi: levis.kavagi@un.org au Jane Nimpamya: jane.nimpamya@un.org.