18 Oct 2019 Tukio Miji

Tunajivunia mashujaa vijana kutoka Kenya wanaotunza mazingira

Tarehe 20 Oktoba, Kenya yasherehekea Siku ya Mashujaa. Siku hii imetengwa ili kusherehekea mashujaa waliopigania uhuru wa nchi. Sisi pia tunatumia siku hii kutambua kazi zinazofanywa na watu binafsi wanaharakati wa mazingira ili kutunza mazingira.

Kote duniani, takribani hekta milioni 12 za msitu huharibiwa kila mwaka. Ukataji wa miti, pamoja na kilimo na madiliko mengineyo katika matumizi ya shamba, vimechangia uzalishaji wa gesi ya ukaa ipatayo asilimia 25.

Ukataji wa miti, pamoja na uharibifu wa ardhi hutoa changamoto kwa hali ya kuweza kustahimili athari za mabadiliko ya tabianchi na kuhatarisha maisha ya familia zinazoishi msituni. Ripoti a Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)inayojulikana kamaGlobal Resources Outlook inaonyesha kuwa matumizi ya mali ghafi yameongezeka kila mahali. Ripoti hii inaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko la asilimia 2.7 la matumizi ya chuma kwa mwaka tangu mwaka wa 1970. Hii inaonyesha umuhimu wa chuma kakita ujenzi, miundo mbinu, uzalishaji na kwa bidhaa za matumizi.

Kuna wajasiriamali watatu kutoka Kenya wanaokabiliana na mazoea ya uharibifu wa ardhi, wanatunza miti na kupunguza ukataji wake.

"Kwa nini vijana?" Kwa kweli, ni kwa sababu vijana ndicho kigezo cha mienendo ya matumizi ya bidhaa kwa sasa na pia watakuwa wafanya maamuzi wa siku zijazo. Kuna matumizi wapya wa bidhaa kati ya bilioni 2 na bilioni 3-wengi wao wakiwa vijana-wanaotarajiwa kuhamia mijini kote ulimwenguni. Kwa kweli, ni kwa sababu vijana ndicho kigezo cha mienendo ya matumizi ya bidhaa kwa sasa na pia watakuwa wafanya maamuzi wa siku zijazo. Kwa hivyo, ni muhimu kufanya kazi na vijana ili wawe na maisha endelevu ambalo ni 'suala jipya la kawaida'," alisema Garrette Clark, Afisa wa UNEP wa Programu ya Maisha Endelevu.

Je una wazo la kipekee litakalowezesha kutunza mazingira? Nafasi ya Tuzo la Vijana Bingwa Duniani itafunguliwa Januari! Tufuatilie kwenye tovuti yetu ili uweze kujisajili.

  1. George Onyango

George mwenye umri wa miaka 23 ni mjasiriamali aliye na maono ya kutumia mapipa ya mafuta kutengeneza viti visivyoathiri mifumo ya ekolojia. Kwa kujali na kupenda mazingira, Onyango hapendi kuona watu wakikata miti.  Hali hii ilimfanya awaze juu ya njia mbadala ya kupata vitu anayotumia kuunda bidhaa zake. Kwa kupenda sanaa na ubunifu, alianza kutumia mapipa ya mafuta kuunda bidhaa za kupendeza. Alianzisha kampuni yake binafsi kwa jina la Drum Furnitures, mwaka wa 2018.

image

Yeye hununua mapipa hayo  kutoka kwa soko la Gikomba, soko linalopatikana jijini Nairobi. Onyango aliamua kutumia mapipa ya mafuta kwa sababu yana sura ya kipee na pia ili kupunguza matumizi ya mbao kuunda fanicha. Fanicha yake ni pamoja na viti, meza na rafu. Bidhaa hivi hutengenezwa vinapoitishwa na wateja.

Kazi ya Onyango ya ujasiriamali imezaa matunda. Matunda hayo ni kama vile kubuni nafasi za kazi, kupanua uelewa wake na kumwzesha kuwa mbunifu. Ana nia ya ya kupanua biashara yake hadi sehemu zingine nchini na hata kuwa na soko la kimataifa katika nchi nyinginezo. Ananuia kutumia ubunifu wake kubuni nafasi zaidi za kazi kwa vijana kila mahali.

  1. Elizabeth Wathuti

Elizabeth ni mwanamke Mkenya mwenye umri wa miaka 23 na mmoja wa vijana kutoka ukanda wa Afrika waliofika kwenye fainali ya shindano la Vijana Bingwa Duniani. Ni mwanzilishi wa mradi wa Green Generation Initiative unaoshughulikia changamoto kama vile za ukataji miti, za mabadiliko ya tabianchi na dhuluma zinazofanyiwa mazingira kwa kuwahimiza vijana wanaharakati wa  mazingira kuchukua hatua za kuyashughulikia, kupunguza baa la njaa, kuwa na elimu nzuri na kuwezesha maisha kwa ardhi.

Amefaulu kufanya haya kupitia kuhimiza shule kutumia nishati isiyochafua mazingira, kutoa elimu kuhusu mazingira, kupanda miche ya matunda ili kuzalisha chakula cha kutosha, na kukuza utamaduni wa kupanda miti miongoni mwa watu ili kuongeza misitu kupitia kampeni ya  “adopt a tree”, na kupitia kwa kuanzisha upanzi wa misitu katika shule mbalimbali.

Kutokana na kujitolea kwa dhati kwa Elizabeth kuyatunza mazingira alipokea ufadhili  kutoka kwa Wangari Maathai Scholarship Award.

  1. Chebet Lesan

Chebet mwenye umri wa miaka 29 ni mwanzilishi mwenza na Afisa Mkuu Mtendaji wa 'Bright Green Renewable Energy'— kampuni ya kijamii inayotengeneza makaa kutoka kwa vifaa vilivyowahi kutumika ili kutunza ekolojia.

Uchomaji wa makaa huchangia katika ukataji wa miti na uharibifu wa mazingira. Kwa kuongezea, makaa yanauzwa bei ghali nchini Kenya. Chebet  alifahamu kuhusu hizi changamoto na akaanzisha kampuni ya kuwapa Wakenya vitu vya kutumia badala ya makaa.

image

Bright Green hutoa kati ya tani 1.5 na 2 za vipande vya matofali ya makaa kwa siku, ambayo ni tani 10 kwa wiki. Vipande hivyo vina manufaa mengi kwa sababu havina moshi, huwaka kwa masaa matatu na huuzwa shilingi  50 za Kenya (dola za Marekani 0.50)  kwa kilo ikilinganishwa na makaa ambayo huwaka kwa saa moja na kuuzwa zaidi ya mara pili ya bei hiyo.

Mchango wa Chebet wa kuhifadhi mazingira kwa kuzalisha makaa yasiyochafua mazingira umezaa matunda. Katika mwaka wa 2017, alitunzwa na Malikia Elizabeth wa pili tuzo la Malikia la Viongozi Vijana kwa kuleta mabadiliko kwa jamii.