Picha: UNEP/Georgina Smith
20 Oct 2022 Video Kushughulikia Mazingira

Jinsi mazingira yanavyoweza kusaidia Afrika kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabianchi

Picha: UNEP/Georgina Smith

 

Ingawa Afrika inachangia kiwango kidogo zaidi ni moja wapo ya kanda zinazoathirika vibaya kabisa na mabadiliko ya tabianchi.  

Kwa mjibu wa ripoti ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) ya Adaptation Gap Mwaka wa 2021, makadirio ya gharama za kukabiliana na hali katika nchi zinazoendelea ni kubwa kati ya mara tano na 10 kuliko usambasaji wa sasa wa fedha za umma za kukabiliana na hali. Inakadiriwa kuwa baadhi ya nchi barani Afrika zitahitaji kuimarisha pesa za matumizi hadi mara tano zaidi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kuliko zitakavyotumia kwenye huduma za afya.  Na gharama za kukabiliana na hali hiyo zinazidi kuongezeka zaidi kwani ulimwengu unashindwa kupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wake wa gesi ya ukaa. 

Barani Afrika, nchi nyingi zaidi zinageukia masuluhisho kutokana na mazingira ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kilimo, iwe ni mawimbi ya joto au kupanda kwa kina cha bahari.  Nchini Gambia, mmoja wa miradi mikubwa zaidi ya maendeleo katika historia ya nchi hiyo ni kuboresha mifumo ya ekolojia ili kuimarisha upatikanaji wa maji ya kilimo. Nchini Tanzania, mikoko imerejeshwa katika ukanda wa pwani ili kutunza uvuvi na mashamba kutokana na kupanda kwa kina cha bahari na mawimbi ya dhoruba. 

Hali ya kutumia masuluhisho kutokana na mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hujulikana kamalimeitwa ‘kushughulikia hali kutegemea mfumo wa ekolojia, na imaweza kuokoa maisha na riziki. Baraza la Kushughulika Mifumo ya Ekolojia ili Kuwa na Chakula cha Kutosha ni mradi wa UNEP wa kuimarisha mifumo ya ekolojia barani Afrika. Linashirikiana na wadau mbalimbali, kuhimiza uwekezaji na kushughulikia nyenzo muhimu, hasa katika mfumo wa kilimo.  Pata maelezo zaidi kwenye video iliopo hapo chini.

 

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa liko mstari mbele kuunga mkono lengo la Mkataba wa Paris la kudhibiti kiwango cha joto duniani kisizidi nyuzijoto 2, na kulenga kufikia nyuzijoto 1.5, ikilinganishwa na viwango vya kabla ya viwanda.  Ili kufikia lengo hili, UNEP imeunda mwongozo wa Masuluhisho katika Sekta Sita, wa kupunguza uzalishaji wa hewa chafu katika sekta mbalimbali kwa kuzingatia ahadi katika Mkataba wa Paris ili kuwezesha kuwa na mazingira thabiti. Sekta Sita zilizoanishwa ni: Nishati; Viwanda; Kilimo na Chakula; Misitu na Matumizi ya Ardhi; Uchukuzi; na Ujenzi na Miji.

UNEP iko mstari mbele kuunga mkono lengo la Mkataba wa Paris la kudhibiti kiwango cha joto duniani kisizidi nyuzijoto 2, na kulenga nkufikia yuzijoto 1.5, ikilinganishwa na viwango vya kabla ya viwanda.  Ili kufikia lengo hili, UNEP imeunda mwongozo wa Masuluhisho katika Sekta Sita, wa kupunguza uzalishaji wa hewa chafu katika sekta mbalimbali kwa kuzingatia ahadi katika Mkataba wa Paris ili kuwezesha kuwa na mazingira thabiti. Sekta sita zilizoainishwa ni: Nishati; Viwanda; Kilimo na Chakula; Misitu na Matumizi ya Ardhi; Uchukuzi; na Ujenzi na Miji. Kongamano la Umoja wa Mataifa la Mabadiliko ya Tabianchi (COP27) mwezi wa Novemba mwaka wa 2022 wlitaangazia kukabiliana na hali, ufadhili na mabadiliko ya haki – na unaweza kutekeleza wajibu wako kwakuchukua hatua sasa kuhusu vitu unavyotumia au kuhamasisha na kuzungumza kuhusu yanayokusumbua.