Miaka 50 ya UNEP

Uwezo na nguvu za UNEP ni kuwa ni taasisi ya kipekee duniani inayoweza kushughulika changamoto sugu za mazingira duniani.

Kwa kindi cha miaka 50 Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) limeratibu juhudi za kukabiliana na changamoto kuu zaidi za mazingira duniani kote. Ushirikiano huu wa kimataifa umesaidia kukarabati tabaka la ozonikukomesha kwa matumizi ya mafuta yaliyo na risasi na kukomesha kuangamia kwa viumbe walio hatarini kutoweka. Uwezo wa UNEP wa kuitisha mikutano na utafiti mkuu wa kisayansi umetoa jukwaa kwa nchi kushiriki, kuchukua hatua dhabiti na kuendeleza ajenda ya kimataifa ya mazingira.

Ili kufanya maadhimisho ya miaka 50 ya UNEP, mfululizo wa shughuli zitaendeshwa mwaka mzima na matukio ya uhamasishaji yanafanyika kufuatia maadhimisho ya UNEP@50. Shughuli hizi zinanatambua maendeleo makubwa yaliyopatikana kuhusiana na masuala ya mazingira duniani na kushughulikia changamoto za sayari zitakazojiri.

Hii inaandaa mazingira a kikao maalum cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA) kitakachofanyika mjini Nairobi, nchini Kenya na mtandaoni, tarehe 3 na 4 Machi, 2022. Tukio hili la ngazi ya juu limetengewa maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa UNEP katika mwaka wa 1972.

Tukio
Tangu mwaka wa 1972, UNEP ni mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira duniani.  UNEP huchochea, huhamasisha na kuelimisha ili kukuza uhusiano…