Taarifa kuhusu COVID-19 zinazotolewa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

Kuambukizwa kwa magonjwa kama vile virusi vipya vya korona vya COVID-19, kutoka kwa wanyama hadi kwa binadamu (zoonoses) ni hatari kwa ukuzaji wa uchumi, kwa wanyama na kwa afya ya binadamu, na kwa utendakazi wa mifumo ya ekolojia. Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa linaunga mkono juhudi za kutunza bayoanuai, kukomesha biashara haramu ya bidhaa za wanyamapori, kudumisha ushughulikiaji mzuri wa kemikali na taka na kuendeleza mipango ya uboreshaji wa uchumi inayojali mazingira na hali ya hewa.

Changia Mfuko wa Kukabiliana na COVID-19.