22 May 2020 Ripoti

Hali ya Misitu Duniani: Misitu, Bayoanuai na Watu

Waandishi: Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO)
Jalada la ripoti

Tulipokuwa tunakamilisha Hali ya Misitu Duniani Mwaka wa 2020 (SOFO), ulimwengu ulikabiliana ana kwa ana na changamoto ambazo hazijawahi kushuhudiwa za janga la COVID-19. Ingawa kipaumbele cha haraka cha kimataifa ni kushughulikia janga hili kwa afya ya umma, mwiitikio wetu wa muda mrefu lazima pia ushughulikie sababu kuu za janga kama hili.

Uharibifu na upunguaji wa misitu ni mojawapo ya sababu zinazochangia na kuvuruga mazingira na kuongeza hatari na kuambukizwa kwa watu kwa magonjwa ambukizi. Kuelewa na kufuatilia hali ya misitu yetu ulimwenguni ina umuhimu sana.