Publication

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Data ya Uharibifu wa Chakula Mwaka wa 2024

27 March 2024
Cover Image

Ili kuimarisha hatua muhimu za kupunguza uharibifu wa chakula na kufikia SDG 12.3, ni muhimu kuelewa kiwango cha uharibifu wa chakula. Kupima uharibifu wa chakula kunawezesha nchi kuelewa ukubwa wa suala hili, na kwa hivyo kuonyesha ukubwa wa fursa, huku miongozo ya kufuatilia hatua zilizopigwa ikiwekwa. Ripoti ya Uharibifu wa Chakula Mwaka wa 2021 ilikuwa nguzo muhimu ya kuwezesha kuelewa uharibifu wa chakula duniani katika sekta za maeneo ya kuuzia, za watoa huduma za chakula, na nyumbani. Iliwezesha upatikanaji mkubwa wa data ya uharibifu wa chakula kuliko ilivyotarajiwa, hasa nyumbani, na kufichua kwamba uzalishaji wa taka za chakula kwa kila mtu nyumbani ulishabiana kote duniani kuliko ilivyodhaniwa hapo awali.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Data ya Uharibifu wa Chakula Mwaka wa 2024 inajengwa juu ya ile ilioitangulia kwa njia tatu muhimu: Kwanza, inajumuisha mkusanyiko wa data pana kutoka kote ulimwenguni, na kutoa makadirio thabiti zaidi ya kimataifa na kitaifa, yaliyofafanuliwa katika Sura ya 2 ya ripoti kamili. Pili, inafafanua mbinu ya kupimia uharibifu wa chakula ya SDG 12.3 iliyoanzishwa katika ripoti ya mwaka wa 2021, huku ikitoa mwongozo ulioimarishwa wa upimaji katika sekta zote za maeneo ya kuuzia, za kutoa huduma za chakula na nyumbani.  Mwongozo huu wa ziada unaangazia mbinu mbalimbali, umuhimu wake na mapungufu yake, na mikakati ya kutoa kipaumbele kwa vipimo kwa sekta ndog, kama ilivyoelezwa katika Sura ya 3.  Hatimaye, ripoti inaacha kuangazia tu upimaji wa uharibifu wa chakula na kuanza kuangazia masuluhisho ya kupunguza uharibifu wa chakula. Sura hii inaelezea mbinu mwafaka za kupunguza uharibifu wa chakula kote duniani, kwa kuangazia ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi katika ripoti hii ya mwaka wa 2024.