Report

Ripoti kuhusu Biashara ya Magari Yaliyotumika Duniani

28 December 2020
jalada

Mamilioni ya magari yaliyotumika, magari madogo na mabasi madogo yanayosafirishwa kutoka Ulaya, Marekani na Japan hadi nchi za kipato cha chini na cha kati yanatinga juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Huchangia uchafuzi wa hewa na mara nyingi huhusika katika ajali za barabarani. Mengi kwayo ni duni na mabofu kuwa barabarani katika nchi zinazoyasafirisha nje.

Ripoti ya kihistoria, ya kwanza ya aina yake ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), inaangazia nchi 146 zinazonunua magari yaliotumika kutoka nje ya nchi na kutoa wito hatua kuchukuliwa kudhibiti biashara hiyo kwa kuweka viwango vya jumla vya chini vya ubora. Hii itahakikisha kuwa magari yaliyotumika hayachangii uchafuzu katika nchi zinazoyanunua. UNEP na washirika watashughulikia masuala haya, kuanzia na mradi unaolenga Afrika.

LINKI MUHIMU

- [Toleo la Habari] Ripoti mpya ya UN inaangazia athari kwa mazingira za magari yaliotumika yaliyonunuliwa kutoka nje ya nchi kwa nchi zinazoendelea

- [Kisa] Magari yaliotumika yatumika tena barani Afrika – kwa gharama zipi?

Mada