16 May 2023 Ripoti

Kukomesha Mtiririko: Jinsi dunia inavyoweza kukomesha uchafuzi wa plastiki na kukuza uchumi unaotumia bidhaa tena na tena

Waandishi: UNEP
Jalada

Ripoti hii inachunguza miundo ya kiuchumi na mashirika ya biashara inayohitajika kukabiliana na athari za uchumi wa plastiki. 

Ripoti hii inapendekeza mabadiliko ya mifumo ili kukabiliana na chanzo cha uchafuzi wa plastiki, kwa kujumuisha kupunguza matumizi ya plastiki iliyo na madhara na isiyohitajika na mabadiliko ya masoko kuwezesha kutumia plastiki tena na tena. Hili linaweza kufikiwa kwa kuimarisha mabadiliko makuu matatu - kutumia tena, kuchakata, na matumizi mapya na matumizi mbalimbali - na hatua za kukabiliana na urathi wa uchafuzi wa plastiki.

Utumiaji tena unarejelea mabadiliko ya ‘uchumi wa kutupa’ hadi kwa ‘jamii ya kutumia tena’ ambapo kutumia tena bidhaa za plastiki ni muhimu zaidi kiuchumi badala la kuzitupa. Ripoti hii inaangazia umuhimu wa kuimarisha soko la kuchakata ili kuchakata plastiki kwa kuhakikisha kuwa kuchakata kunakuwa mradi wa manufaa zaidi.

Matumizi mapya na matumizi mbalimbali inarejelea kufanyia mabadiliko masoko ili yawe na njia mbadala endelevu kwa plastiki, ambayo itahitaji mabadiliko kwa mahitaji ya watumiaji, kwa mifumo ya kisheria na kwa gharama. 

Ripoti hii inaangazia kuwa masuluhisho haya yanapatikana kwa sasa na kwamba mabadiliko ya mifumo, yakiambatana na sheria mwafaka, vitapelekea manufaa mbalimbali ya kiuchumi na kupunguza madhara kwa afya ya binadamu, kwa mazingira na  kwa hali ya hewa.

Dunia inawezaje kukomesha uchafuzi wa plastiki?

Mabadiliko ya kimfumo yanahitajika ili kukabiliana na sababu zinazozopelekea uchafuzi wa plastiki. Inajumuisha kupunguza matumizi ya plastiki inayosababisha matatizo isiyohitajika na mabadiliko matatu katika masoko – Kutumia tena, Kuchakata, na Matumizi mapya na Matumizi mbalimbali – na juhudi za kukabiliana na urathi wa plastiki.