05 December 2023 Ripoti

Ufuatiliaji wa Upunguzaji wa Joto Duniani Mwaka wa 2023

Waandishi: UNEP
Jalada

Ripoti ya Ufuatiliaji wa Upunguzaji wa Joto Duniani inaonyesha uwezekano na njia za kutozalisha hewa chafu kutoka kwa sekta ya kupunguza joto. Kwa kutumia modeli iliyoundwa mahususi kwa ripoti hii, inawasilisha njia kutozalisha hewa chafu kutoka kwa sekta kuu za kupunguza joto na inatoa wito kwa nchi kuchukua hatua kwa kufuata sera na mikakati ambayo ina athari kubwa zaidi katika kupunguza uzalishaji wa hewa chafu unaotokana na mifumo ya kupunguza joto na kufanya watu wote kupunguza joto kwa njia endelevu.

Ripoti ya Ufuatiliaji wa Upunguzaji wa Joto Duniani, Kudumisha Ubaridi: Jinsi ya kukidhi mahitaji ya kupunguza joto huku tukipunguza uzalishaji wa hewa chafu kutoka kwa muungano wa Cool Coalition unaoongozwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa – inaainisha hatua endelevu katika maeneo matatu: mifumo ya kupunguza joto isiyohitaji ukarabati, viwango bora vya kutumia nishati vizuri na hatua za dharura za kuachana na friji zinazoongeza joto. Ripoti hii inayotolewa ili kuunga mkono Ahadi za Kupunguza Joto Duniani, mpango wa pamoja kati ya Muungano wa Cool Coalition na Umoja wa Falme za Kiarabu kama mwenyeji wa COP28. 

Ripoti ya Ufuatiliaji wa Upunguzaji wa Joto Duniani: Kudumisha Ubaridi

Iwapo hatua zilizoangaziwa katika Ripoti ya Ufuatiliaji wa Upunguzaji wa Joto Duniani Mwaka wa 2023: Ripoti ya Kudumisha Ubaridi zitatekelezwa ipasavyo, tunaweza kuzuia joto kuzidi katika ulimwengu unaoshuhudia ongezeko la joto.

Njia tano ambazo miji inaweza kudumisha ubaridi huku ikipunguza uzalishaji wa hewa chafu

Kutolewa kwa Ripoti ya Ufuatiliaji wa Upunguzaji wa Joto Duniani Mwaka wa 2023: Kudumisha Ubaridi inaonyesha umuhimu wa njia mbadala za kzisizohitaji ukarabati za kupunguza joto badala ya viyoyozi vinavyotumia umeme mwingi. Ripoti hi iliyotolewa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), inaeleza kuwa kati ya sasa na mwaka wa 2050 vifaa vya kuppunguza joto duniani…

Kwa nini nchi zinatafakari kuhusu "ahadi ya kupunga joto" katika kongamano la mazingira la Umoja wa Mataifa

Viongozi watakapokutana wiki hii kwa Kongamano la Umoja wa Mataifa la Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) wataombwa kutia saini mkataba wa kupanua upatikanaji wa huduma na teknolojia endelevu za kupunguza joto, msukumo unaotokana na mwaka wa 2023 kuwa mwaka ulioshuhudia kiwango cha juu cha joto.