21 October 2021 Ripoti

Kuanzia kwa Uchafuzi hadi kwa Masuluhisho: tathmini ya kimataifa ya uchafu wa baharini na uchafuzi wa plastiki

Waandishi: UNEP
img

Kuanzia kwa Uchafuzi hadi kwa Masuluhisho: Tathmini ya kimataifa ya uchafu wa baharini na uchafuzi wa plastiki inaonyesha athari za uchafu kwa mazingira na athari zake kwa mifumo ya ekolojia, kwa wanyamapori na kwa binadamu.

 

Plastiki hushikilia nafasi kubwa ya uchafu hatari zaidi na sugu baharini, ikikadiria asilimia 85 ya taka za baharini.

Tathmini hii inaangazia kiwango na madhara ya uchafu wa baharini na uchafuzi wa plastiki na kuchanganua masuluhisho na juhudi zilizopo. Tathmini hii inaonyesha kuwa hatari kutoka kwa takataka za baharini na uchafuzi wa plastiki yzinaongezeka katika mifumo yote ya ekolojia kuanzia kwa chanzo hadi kwa bahari. Inazungumzia kwa kina kuhusu utafiti wa sasa (na mapungufu ya maarifa) kuhusiana na athari za moja kwa moja kwa viumbe vya baharini, hatari kwa mifumo ya ekolojia na afya ya binadamu, na gharama kwa jamii na kwa uchumi.

Kwa ujumla, tathmini, ambayo inakusudiwa kuwezesha hatua zinazozingatia utafiti katika ngazi zote, inasisitiza umuhimu wa hatua za dharura kote ulimwenguni. Inaonyesha kwamba ingawa tuna maarifa, tunahitaji kujitolea kwa wanasiasa na hatua za dharura ili kukabiliana na changamoto hizi zinazoongezeka. Ripoti hiyo itaongoza majadiliano katika Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA 5) mwaka wa 2022, ambapo nchi zitakusanyika ili kuamua hatima ya kuendeleza ushirikiano wa kimataifa.

 

Rasimali Zaidi:

Uliza Mwanasayansi

Pata elimu kutoka kwa mwanasayansi maarufu na mwandishi mkuu kuhusu uchafu baharini, anayeathirika na tunachoweza kufanya ili kupunguza kiwango cha uchafuzi baharini.

Measuring ambient water quality. SDG Indicator 6.3.2.

Video hii inaangazia umuhimu wa kufuatilia na kutathmini ubora wa maji katika mito, maziwa na vyanzo vya maji ulimwenguni na kuisimamia na kuitunza. Pia inasisitiza kwamba kwa vyanzo vingi vya maji tunavyovitegemea kuishi na kupata riziki zetu kuna mapungufu makubwa ya data, haswa katika nchi masikini.

Implementing Integrated Water Resources Management: SDG Indicator 6.5.1.

Shinikizo kwa rasilimali za maji linaongezeka kwa njia isiyokuwa endelevu. Usimamizi Anuai wa Rasilimali za Maji (IWRM) huleta watu kutoka sekta zote pamoja ili kuhakikisha kuwa rasilimali za maji zinasimamiwa kwa uendelevu, kwa njia ya haki na kwa ufanisi. Iwapo tunataka kufaulu kuwa na ulimwengu bila ubaguzi kufikia mwaka wa 2030, tunahitaji kuongeza mara dufu kiwango ambacho…