06 February 2023 Ripoti

Ripoti Inayotolewa Kila Mwaka ya Mwaka wa 2022

Waandishi: UNEP
Jalada la ripoti

Katika mwaka wa 2022, athari mbaya za changamoto za aina tatu duniani zilizidishwa na kuongezeka kwa ukosefu wa usawa, mizozo na kupanda kwa bei ya chakula na nishati. Hata hivyo, ulikuwa pia mwaka wa mwamko mpya wa kuchukua hatua za kushughulikia mazingira.

 

UNEP iliadhimisha miaka 50 tangu nchi zipitishe mikataba ya kimataifa ya kuzuia uchafuzi wa mazingira, kutunza na kuboresha bayoanuai, na kusaidia mataifa yaliyo hatarini zaidi kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi. Lakini kazi kubwa ilioko mbele yetu ni kupunguza kwa dharura majanga kwa sayari. Kama mamlaka kuu duniani ya kushughulikia mazingira, UNEP inatoa kipau mbele kwa kufanya kazi na Nchi Wanachama na wabia ili kutoa masuluhisho endelevu kwa manufaa ya watu na sayari. Tazama ilivyo katika ripoti ya mwaka huu.