Aquaman
UNEP ilimtangaza nyota wa Aquaman na mwanaharakati wa masuala ya bahari Jason Momoa kama Mhamasishaji mpya wa Maisha Chini ya Maji katika Kongamano la Umoja wa Mataifa la Bahari.
UNEP ilimtangaza nyota wa Aquaman na mwanaharakati wa masuala ya bahari Jason Momoa kama Mhamasishaji mpya wa Maisha Chini ya Maji katika Kongamano la Umoja wa Mataifa la Bahari.
UNEP ilitoa Tuzo kwa Sir David Attenborough Tuzo la Mabingwa wa Dunia katika kitengo cha Mafanikio ya Kudumu kutokana na kujitolea kwake kupitia utafiti, uhifadhi wa kumbukumbu na uhamasishaji kuhusu utunzaji na uboreshaji wa mazingira.
Ripoti ya Hali ya Fedha za Kufadhili Mazingira Mwaka wa 2022 ya UNEP ilibainisha kuwa serikali, mashirika ya biashara na taasisi za fedha zinahitaji kuongeza uwekezaji wao wa kila mwaka mara tatu zaidi ili kudhibiti ongezeko la joto duniani, kukomesha kupunguza uharibifu wa bayoanuai, kukomeha uharibifu wa ardhi na kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu.
Katika mwaka wa 2022, UNEP ilijiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuimarisha juhudi za kukabiliana na changamoto za aina tatu duniani kwa kushughulikia afya ya binadamu, wanyama, mimea na mazingira kama changamoto moja iliyounganishwa.
Azimio hilo litasaidia kupunguza uasi kwa mazingira, kuziba mapengo ya ultunzajii na kuwawezesha watu hasa walio katika mazingira hatari wakiwemo watetezi wa haki za mazingira, watoto, vijana, wanawake na watu wa kiasili.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres
Mwezi wa Julai, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza upatikanaji wa mazingira safi, bora na endelevu kuwa haki ya binadamu wote. Mafanikio hayo yalikuwa kilele cha kazi ya miongo mitano, ambayo ilianza Azimio la Stockholm la 1972, na uhamasishaji usio na kikomo kutoka kwa UNEP, maelfu ya mashirika ya uraia na makundi ya watu wa kiasili.
Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia, unaosimamiwa na UNEP na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), unasaidia kutekeleza ahadi za kuboresha hekta bilioni 1 za ardhi, eneo lenye ukubwa sawa na China, kufikia mwaka wa 2030. Mwaka wa 2022, Muongo huo ulituza Miradi 10 za kwanza Anzilishi za Kuboresha Mifumo ya Ekolojia Duniani, zinazolanga kuboresha zaidi ya hekta milioni 68 - eneo kubwa kuliko Myanmar, Ufaransa au Somalia - na kubuni nafasi za kasi takribani milioni 15.
Katika mwezi wa Desemba, katika Kongamano la Umoja wa Mataifa la Bayoanuai (mkutano wa 15 wa Kongamano la Nchi Wanachama wa Mkataba wa Uanuai wa Kibayolojia - COP15), Mataifa yalikubaliana juu ya mfumo mpya msingi wa kutunza bayoanuai - Mfumo wa Kimataifa wa Bayoanuai wa Kunming-Montreal, ukiwa na malengo manne na shabaha 23 za kupunguza uharibifu wa bayoanuai kufikia mwaka wa 2030. Shabaha - ambazo nyingi zinalenga kuimarisha haki za watu wa kiasili, ambao ni wasimamizi wakuu wa bayoanuai - ni pamoja na:
Katika mwaka wake wa kwanza, Kituo cha Kimataifa cha Kufuatilia Uzalishaji wa Methani Duniani (IMEO) cha UNEP kilitekeleza wajibu muhimu kusaidia kupunguza uzalishaji wa methani, kichocheo cha pili kwa ukubwa cha ongezeko la joto duniani. Kituo hiki kilianzishwa ili kusaidia kufikia malengo kama vile Ahadi za Methani Duniani za kupunguza asilimia 30 ya uzalishaji wa methani katika sekta ya mafuta na gesi, sekta ya kilimo na taka kufikia mwaka wa 2030.
Huku nchi zinazoendelea zikitarajiwa kuongeza magari bilioni 1 kufikia mwaka wa 2050, juhudi zinahitajika ili kuhakikisha magari hayo mengi yanazalisha kiwango cha chini au kutozalisha gesi chafu.
Chapisho hili linaweza kunakiliwa lote au sehemu yake na kwa namna yoyote kwa madhumuni ya elimu au yasiyokuwa ya biasharaa bila ruhusa maalum kutoka kwa mmiliki wa hakimiliki imradi unaonyesha chanzo chake. Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa litafurahia kupokea nakala ya chapisho lolote linalotumia chapisho hili kama chanzo. Hairuhusiwi kuchapisha chapisho hili ili kuliuza tena au kwa madhumuni mengine yoyote ya kibiashara bila kibali kupitia maandishi kutoka kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa. Uteuzi wa mashirika kijiografia katika ripoti hii, na uwasilishaji wa makala humu, haimaanishi utoaji wa maoni ya aina yoyote kwa upande wa mchapishaji au mashirika yanayoshiriki kuhusu hadhi kisheria ya nchi yoyote, kanda au eneo, au ya mamlaka yake, au kuhusu uwekaji wa mipaka yake. Wa Kumtaja: Isipokuwa imeonyeshwa vinginevyo, data yote katika chapisho hili imetolewa kutoka kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa. Kwa taarifa zaidi: unep.org/annualreport.
© Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, 2023