Kongamano la Umoja wa Mataifa la Bayoanuai (COP 15)

Mazingira na bayoanuai vinadhuriwa kutoka kila upande.  Na binadamu analipia kwa kumsaliti rafiki yake wa karibu.  Kwa maneno ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, "tunajiua kwa kuyadhuru".  Kongamano la Nchi Wanachama lazima lidumishe mustakabali wa mfumo wetu wa maisha kwenye sayari.

Desemba 7-19, 2022 MJINI Montreal, Canada, serikali kutoka pembe zote za duni zilikuja pamoja kukubaliana kuhusu malengo mapya ya kuangoza ulimwengu kuchukua hatua kufikia 2030 za kusitisha na kukabiliana uharibifu wa mazingira.

Mazingira is muhimu ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu na kudhibiti ongezeko la joto duniani lisizidi nyuzijoto1.5. Kupitishwa kwa mfumo wa kimataifa wabayoanuai unaoshughulikia vichochezi vikuu vya uharibifu wa mazingira ni muhimu ili kudumisha afya na ustawi wetu pamoja na ya sayari.

Ni yepi yaliojiri kwenye COP 15:

  • Kupitishwa kwa mfumo wa usawa na wa kina unaolingana na rasilimali zinazohitajika kuutekeleza
  • Malengo yanayoeleweka kwa wazi ya kukabiliana na matumizi kupita kiasi, uchafuzi, ugawaji wa ardhi vipande vipande na kilimo kisicho endelevu
  • Mpango unaolinda haki za watu wa kiasili na kutambua michango yao kama wasimamizi wa mazingira
  • Ufadhali wa bayoanuai kwa kuoanisha na mtiririko wa fedha na mazingira ili kuwezesha uwekezaji endelevu na kuachana na ule unaodhuru mazingira.